February 14, 2018

HARUFU YA PILAU LA MAMA BONI ILIWAVUTA ASLAY NA NANDY.

NA HONORIUS MPANGALA
Ni mwendo wa Kilometa 30 kutoka Mlandizi ili ufike Kijiji cha Matimbwa. Pia ni kilometa 8 ukitokea Bagamoyo Mjini ili ufike hapo kijijini. Ilinichukua masaa yasiyo zidi manne kutoka Morogoro hadi nafika kijijini hapo. Yawezekana ikawa ni jina la kijiji ambacho wengi wao wasiweze kukifahamu kama ilivyo Msata katika wilaya hiyo ya Bagamoyo. Ni eneo la jimbo la mheshimiwa Shukuru Kawambwa. Wakazi wake wengi wakiwa Wazaramo,huku Wakwere nao wakiwepo kwa kiasi.
Nyumba mojawapo iliyoko katika video ambapo Nandy kaonekana kaegemea kwenye ukuta huku akiimba
Wakati napanda gari Mlandizi wenyeji wangu Mathayo Venance na Saidi Zimbwe wakanipa maelezo shukia kituo cha Matimbwa Magengeni. Nilikuwa na shauku ya kuijua Matimbwa na Bagamoyo kwa kweli na nilifika salama na kufanya kazi yangu vyema. Jambo kubwa ninalotaka kuwajuza sio mimi nilisafiri vipi kufika huko. Bali nataka nikupe umaarufu wa Matimbwa ambao hata mtayarishaji wa picha mnato Hans Cana autambue vyema.

Ni katika picha mnato ya wimbo wa ‘Subakheri mpenzi’ ulioimbwa na Aslay na Nandy ulimfanya mtayarishaji Hans Cana awapeleke Kijiji cha Matimbwa na kufanya video huko. Kama umjuavyo msanii Aslay huwa mtu wa kupenda picha mnato ambazo hupendwa na watu wa viwango vyote vya Maisha. Hupenda kufanya video akiwa kijijini na huvaa uhusika haswa uhalisia Wa mazingira. 
Pikipiki iliyotumika katika wimbo wa Subakheri Mpenzi


Awali sikulifahamu hilo kwa Nandy lakini katika picha mnato hii nikiri wazi naye ni mmoja wale ambao huweza kuhusika vyema popote kwa mazingira ya mjini au kijijini. Wakati Aslay na timu yake ya kuchukua picha mnato wa wimbo huo ilipofika kijijini hapo wakanusa harufu ya Pilau lililokuwa likiivishwa katika mgahawa mmoja hapo Matimbwa magengeni. Ulikuwa mgahawa Wa mama Regina Shija almaarufu kama mama Boni.
Harufu ya pilau ikamfanya Nandy awe Wa kwanza kusogelea mgahawa huo. Kitu pekee alichokifanya Nandy ni kuingia hadi jikoni na kumwomba Mama Boni ampatie pilau lenye samaki na mboga za majani. Hiyo ikawafanya na wengine kusogea hapo kama Hans Cana na timu nzima kuagiza pilau hilo. Wakati chakula kikiendelea ndipo Nandy alipokiri kuwa aliisikilizia harufu ya pilau akiwa mbali na mgahawa huo ikabidi asogee hapo.

Wakiwa chini ya kiongozi Wa kiongozi Wa kikundi cha ngoma Vanga bwana Kondo Milonge kila kitu kilienda sawa. Katika picha mnato ya wimbo huo kuna pikipiki ambayo anaonekana Aslay kaikalia ambayo ni ya aina yake. Ni pikipiki ambayo iko katika mfumo Wa gari na hiyo yote ni kazi ya mmiliki ambaye ni Fundi pikipiki kijijini hapo.

Ile pikipiki ni ufundi wa Fikiri Gombe almaarufu kama Magoso. Nafikiri wengi mtakuwa mmetambua kwanini Fikiri kapewa jina la Magoso ni kutokana na mchezaji Wa zamani Wa Simba aliyeitwa jina la Fikiri Magoso. Mwonekano Wa ile pikipiki ulimfanya Hans Cana ahitaji kuitumia katika kazi yake. Ina usukani kama Wa gari,Krachi yake inakanyagwa kama ya gari,hata gia pia hutumia mkono kuingiza na kutoa. 

Ni upande wa mafuta tu ambao uko sehemu yake kama zilivyo pikipiki zingine ila haufabani kwa mwonekano kwani badala ya kunyonga yeye Magoso alitengeneza mfumo Wa kukandamiza kwa kiganja chake.Hiyo ndo pikipiki ya Fundi Fikiri Gombe almaarufu kama Magoso.
Nikiwa natoka kupata madafu toka kwa baba yake Ferouz,picha tuliyokuwa pamoja sijaiweka kwasababu ya kutoruhusiwa naye. Pembeni yangu Mwite Hakimu rafiki yangu tuliyekutana huku. 

Vanga halikuachwa nyuma katika picha mnato hii na ikaonekana Nandy na Aslay wakilisakata haswa haswa. Ilikiwa ni nyumbani kwa Kondo milonge aliyeshirikiana na wana kikundi wenzake kuhahakikisha kipande chao kinaenda sawa. Unajua Aslay ni mtu wa masihara sana katika jamii,anapenda utani. Sasa wakati Wa mchana walipita katika mji anaoishi Dada mmoja aitwaye Zalfa Kessy wakiwa wanaenda kumalizia sehemu yao ya mwisho ya kurekodi picha mnato hiyo. 
Katika kipande ambacho Nandy kaonekana kasimama akiwa ameegemea ukuta Wa nyumba huku akiimba,sasa mita chache ndio kuna Nyumba anayoishi huyo Bint Kessy. Aslay akakaribishwa chakula hapo jamaa 'hakuvunga' akajisogeza na mmoja ya watu aaliotanguzana naye na wakala chakula katika hali ya kawaida kabisa. Wanaposema ishi kulingana na mazingira basi huyu kijana naweza kusema ana nyendo kama za Juma Kassim almaarufu Juma Nature.

Ukitaka kujua uhusika wa watu katika picha mnato za wenzetu wa mataifa mengine huwa wanalipwa. Kitendo cha kutoka katika video lazima ulipwe kwa kile utakachokifanya. Lakini yawezekana hapa kwetu Tanzania hali ikawa tofauti na inavyofikiriwa.

Katika picha mnato hiyo wako waliolipwa kutokana na kupangwa mapema uhusika wao. Lakini wako ambao hawakulipwa na waliridhika kwa mioyo yao vitu vyao au nyumba zao zitumike na mambo kwenda bila taabu yeyote. Yawezekana mwonekano wa Aslay na jinsi alivyoifanya picha mnato hii kuwa ya mazingira ya kijijini ndo ulipelekea hata wanakijiji waone haina haja ya kumtoza chochote. Walijiuliza kaacha vijiji vingapi hadi aje Matimbwa?

Huu ndo Utanzania ambao mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaachia Watanzania. Kuishi kijamaa kuonana tuko ssawa kama katiba yetu inavyoeleza.
Licha ya hayo yote kufanyika hapo lakini kumbe baba aliyemzaa msanii Feruoz anaishi kijijini hapo.Hata msaani maarufu Wa muziki Wa Dance Muumini Mwinjuma anatokea huko. Nikionyeshwa dad yake Muumini akiyeolewa hapo kijijini pia.Unaambiwa hata marehemu Banza Stone alikuwa mwenyeji sana Matimbwa.

Hiyo ndiyo Matimbwa ya Wazaramo ambayo Mtayarishaji Hans Cana aliamua kumpeleka Aslay na Nandy kwenda kufanyia picha mnato ya wimbo Wa Subalkheri mpenzi.

Waweza ingia katika mtandao kama YouTube na kujionea maandalizi ya picha mnato hii na ukajionea Mengi zaidi ya niliyoeleza. Si unajua 'behind the Scene' ndo pahala ambapo watu huweza jione kila jambo lililojiri katika utayarishaji Wa picha mnato ya filamu au wimbo.
0753 44 92 54

No comments:

Post a Comment

Maoni yako