August 20, 2007

Fomu za Big Brother ilikuwa moto?

Heee! inaweza kuwa ngeni hata kwangu lakini ndio ukweli kwamba uchukuaji wa fomu za kushiriki katika shindano la Big Brother Afrika ilikuwa moto mkali sana,

Hebu tafakari Salama Jabir(EATV),Tayana(Clouds FM)Witness(Wakilisha) na wengine,ama ilikuwa bonge la ushindani.Lakini mwishowe kijana Richard akaibuka kinara,kwanini?Najiuliza sana hapo, imekuwa dada zangu hao kutoswa?kulikoni hawa waendashaji?Duuu! kwa maana hiyo wanahitaji mtu asiyefahamina au siyo,

Jamani hebu fananisha ujulikanaji wa akina dada hao na huyu mchizi wangu Rich we acha tu yaani maajabu.

Lakini naamini kwamba kijana atafanya zaidi ya mwenzetu 'Mwisho Mwampamba' mwenye bonge la jina la kitanzania!upo hapo...hebu soma jina la mwakilishi huyo wa 2003.

OOh bahati mbaya mwaka huu sijawa mtazamaji kama shindano la kwanza hii ni kutokana na kupoteza kitu fulani katika shindano la mwaka huu,yaani kwa mtaalamu wa vitu aliyeona lililopita 2003 kwa hili ataona kama mdoli tu na ndivyo nilionavyo,maana wamepelekwa wazee watupu tazama umri wao....

aaaah ni porojo tu burudani

Ingia katika tovuti yao ya www.mnetafrica.com

4 comments:

 1. hakuna shida bwana kupenda sehemu ni bora tu hivyo kazana sana

  ReplyDelete
 2. yaani nashindwa kuelewa kwanini hawa jamaa wanakuwa na siri kali namna hii.unakumbuka kwa ile ya bodea,yaani ikawa siri tupu.
  tusaidieni hapo kuwahoji.

  ReplyDelete
 3. siyo siri hadi salama kapigwa chini,tayana naye,ama kweli hili shindano linahitaji watu wasiojulikana kabisa

  ReplyDelete
 4. kama mambo yote yangekuwa hivi basi hakuna atakayejiona yuko juu ya mwenzie maana kwa shindano hili fomu zake kama vita

  ReplyDelete

Maoni yako