August 14, 2007

NDESANJO MACHA NIMEKARIBIA BLOGUNI

Eeee hakuna ubishi tena kwamba kama ni hamu ya kula sasa naweza kuwa na hamu zaidi ya mwanzo. Ndugu yangu pamoja na kusema polepole ndio mwendo,lakini leo naona ni wakati wa kukupatia ukweli kwamba nimekaribia hasa katika mtandao wa wakubwa,na nashukuru kwa kunipa maarifa haya huku pembeni yangu kukiwa na kijana machachari aliyenifundisha pia jambo hili ndugu Simon Regis yaani we acha tu.

Lakini usistaajabu kwani nimetumia nafasi hii leo kuwapasha na kupayuka kwa ukali kwamba nimekuja kamili kama mchawi na dhana za kivita yaani mizizi n.k
lakini jamii isinielewe vibaya kwani kila jambo lina wakati wake hivyo ni vyema tukafahamisha furaha,vcheko na mambo mengine yahusuyo maisha yetu.

Lakini jambo la msingi kwangu ni kwamba huu ni wakati wa kuwakilisha mambo mapya ya teknolojia ya habari. Tupo katika nyanja nyingine za habari maana ni wakati wa kuachana na makaratasi ya kuwabana mbavu wanahabari wetu na vyombo vya habari vya uwongo na barua zao za wasomaji.Hapana sina wakati wa kuwalaumu bali ni wakati wa kuwaeleza kile kilicho bora zaidi.

Haya na bunge lunu huko wapi sijui linafanya vikao vya kuwasaidia masikini wetu kama akina mimi ili tuondokane na kuombaomba mmmmhhh.makubwa!Karibuni katika balaza la mtoto wa kinyasa kutoka kijiji cha Lundu,familia ya akina Mpangala

No comments:

Post a Comment

Maoni yako