August 15, 2007

Ni siku nyingi sana bado nawaza namna ambavyo umekuwa ukisumbua akili yangu.Lakini kwa hakika nimejitahidi kutafakari mambo mengi katika mustakabali wa maisha yangu tokana na njia yako uliyopita,hata hivyo jibu ni kwamba sina wakati wa kupoteza katika maisha na mtazamo wangu ulivyo sas na mtazamo mpya ninaoujenga ni hatari kughilibiwa!ipo kazi ndugu zanguni maisha haya jamani......

Msomaji unaweza kudhani ni lawana haba lakini ni nyingi kuliko jinsi ambavyo msichana huyu alivyofanya.Pia siwezi kulaumu lolote kuhusu maamuzi yake na mwenendo wake wa maisha,lakini anapaswa kutazama upya,kwani siafiki mtazamo huo ndio maana tunahitilafiana.

Msichana huyu aitwaye YASINTA ni msichana ambaye tulikua pamoja toka sekondari mkoani kwangu Ruvuma,nilijikuta nikiamini kwamba ukiwa na msichana ni bonge la ujiko kumbe ulikuwa ujuha tu.Wacha niseme msomaji wangu ni mbaya sana ukawa na mtu ambaye unampenda halafu ukaachwa njiani kwa sabau tu kuna tofauti za mtazamo ambazo haziwezi kufanana hivyo mnakubalina kidogo na mnatofautiana sana,hivi unatarajia nini?

Basi ikawa kama ni ujiko ambao hata hivyo ulinisaidia kwa kipindi kifupi tu,kwani wakati huo 1999-2000 hadi nilipo maliza kidato cha nne 2001 nilikuwa tayari nimejikwaa kidogo lakini niliamini ipo siku yanaweza kujirudia masuala yale,ambayo nilidhani ni mema.Kwa kawaida vijana wengi hupenda sana ujiko hasa tukiwa mashuleni ambako tunajumuiya za wanafunzi wa aina mbalimbali hivyo kila mmoja anajitahidi kuonyesha umahiri wake wa masuala kadhaa.

Kwangu kuwa na msichana mwanzo lilikuwa jambo gumu sana lakini kwa huyu ilitokea kwa nia ya ujiko hapo shule,hata hivyo bado najiuliza mbona nina maumivu mimi kuliko yeye alivyofanya?Kifupi ni kwamba imefikia wakati binadamu kutazama upya mitazamo yetu juu ya masuala haya ya mapenzi,tunahutaji kuweka kanuni imara ili ukichanganua mlinganyo wa maisha yako ubaini kwamba kama ulikosea kanuni basi lazima majibu yatakugomea tu.

Sasa wakati narejea rejea kisa hiki ambacho kwa kweli kinanichanganya sana kukitatua kwasababu nhusika sinaye karibu,huwa nachanganya sana hoja zangu hilo mnisamehe sana.
Ni hivi msichana huyu tulijumuika pamoja enzi hizo tukiwa shule LUNDO SEKONDARI(kwa waliofika Mbamba Bay au Liuli wanaifahamu).Nilikuwa kama nimeona dunia yote yangu nikajiona bonge la mjanja huku nikiwa na ka umaarufu fulani kwanza nilikuwa mchezaji wa "volleyball" mkali na ambaye alifundisha wengi pale shule,usishangae ujiko huo.

Msichana huyu basi akawa hanijui wala kuniaona najichanganya na watu wengi isipo kuwa rafiki yangu mkubwa wakati huo Simon Haule na niliokuwa na urafiki wa maarifa sana kama Michael Mkate na Libaga Mapunda(wanisamehe kwa kuwataja) au nikiwa pale bweni nakula muda mzuri wa kusoma vitabu kama "kikosi cha kisasi" n.k.Huyu rafiki yagu wa kwanza alikuwa mtu wa "vidosho" sana hivyo hatukuweza kulingana katika falsafa na itikadi lakini wawili wa mwisho hapo juu nilikuwa nao bega kwa bega katika kusaka maarifa kwa njia za kikoloni.

Basi kijana nikawa na matokeo mema darasani na hapo ndipo huyu ninayemwandika leo akajitokeza kwangu kwa kudadisi hivi mimi ni nani na natokea wapi.Wengi walijua kijana nimetokea pale Mbinga mjini kumbe wapi kijana pale nilikuwa nakula muda mzuri wa mapumziko ya baada ya shule kufungwa.Naam... tukazoeana kidogo kama ujuavyo akinadada kwa mikogo,wala kijana sikuwa na mchecheto kwani nilikuwa najiamini utadhani Hitler(usiogope) yaani nilijiona gangwe kama Okonkwo,nilikuwa na kasumba za kutojiunga na makundi yasiyo na jipya wala mtazamo wowote wa maisha,nilijiona natafuta maarifa kwa nguvu za kibitozi tui lakini sikua na hata kauchembe ka huo unini.....

Ilikuwa kama mzaha tu kwa msichana kama huyu ambaye alichukuliwa na wanafunzi kuwa wa hadhi ya juu si uanajua tena vijana wa shule.Ikawa mchana ,ikawa siku basi maua tukayapanda wenyewe.Tukaendelea hivyo hadi pale kisanga ambacho amekuwahi kuniuliza kwanini nilifanya vile.Kisanga hicho kilitokea nikiwa katika kambi ya UMISETA yaani duu!haya ikawaje?kisanga kikaishia hapo(sitakisema) naona haya. Ni hivi nilishangaa mtoto kawa kama kavurugwa akili na jambo fulani ila roho ikawa inampwita aanzeje maana baada ya kambi hiyo kumalizika na wachezaji kuruhusiwa kurejea mashuleni kwetu ikawa kama kawaida kufika Mbinga toka Songea kijana nikaona ngoja nionane kwanza na washikadau wangu ili nikija likizo wajue kijana alikwisha kuwapatia jambo langu muhimu la likizo hiyo.

Lakini huko shule binti akawa anasubiri kijana nije,lakini si kama mwanzo bali ni kama kuunganisha UJAMAA na UNYANG'AU(ubepari),ilikuwaje? Niligundua siku moja hivi maana si unajua kwamba ukisoama vitabu vyenye akili unapata mwanya wa kuchanganua mambo? Nilipobaini jambo sikuhoji nilinyamaza tu huku kijana wangu wa kazi(rafiki)Godfrey Christopher akinipa habari nzima basi nikasema mimi ni ngangari nitalimaliza kijeuri!lakini wapi,.ikawa kama nachelewa tu kwani alitakiwa kunieleza kitambo lakini aliposuasua nami nikala jiwe tu kusubiri nini kitajiri ili kuokoa muda.

Lakini kumbuka kwamba yalioyojiri wakati ule tayari nilishatemwa kikosini na nilijaribu kujirejesha katika kiwango changu ikashindikana,tukabaki kupiga stori za hapa na pale na WATU wasijue kama hakuna tena ujiko kama wa kale,tukabaki kuwa marafiki kama ilivyoada kwa binadamu sote ni ndugu.ikawa mchana ,ikawa usiku mambo hayakubadilika nikakukabli matokeo kwa kauli kwamba ipo siku tutaonana na tutajiuliza sababu pia kwamba mimi ni mtu sahihi kwake kuliko wengi wanaomtazama kama chui mwenye uchu wa kula nyama.

2006 hiyo kijana nipo jiji la matapeli DAR naona na binti lakini hii ni baada ya kutoonana kule Mbeya na nyumbani mkoani hapa Ruvuma hususani kijiweni kwangu Mbinga mjini ambapo yeye ni makani yake tofauti na mimi toto la kinyasa la kuvua samaki wa kitoweo;tunajaribu kusahihisha kwanini sisi tulifarakana hatua ile?(kutemana)lakini jibu likawa nani alianza?tuhuma kibao mara kijana anayeandika hapa alikuwa ana kimada kwa siri.Jibu la mwisho kijana anayeandika hapa akasema msichana ndiye aliyeanza na hoja hii ikakubalika,tatizo ni kwamba tulidhani ni wakati wa kufanya kweli sasa kwasababu tumekuwa angalau umri wa kati kama 10+10+3= sijui nini huko! kwamba muda wa kuwa pamoja kwa umakini.eeeeeeeeeeeeeeehhhh wapi bwana yaani ni balaa tupu,nashusha aya.......

Siku moja nikapokea sauti ya kutisha toka katika simu kisha ujumbe wa simu ukaingia baada ya mazungumzo na kijana aliyenihoji kuwa mimi ni nani.Duu nikajua kwamba nimeingia anga mbaya kwa kuruhusu mtu aliyeimwaga enzi hizo eti sasa nione chungu kapata kivuno...........,.,,,.Nikaambiwa kwamba huyu ndio "waubani" wake hivyo nisitume ujumbe wala kubipu si mnajua za kibongo kwa kubipu.Lakini hii ilikuja baada ya kutoonana kwa miaka 3 kwani hata huo 2006 ulikuwa wa 4 nikaona iwe vyema ninyamaze....AAh hapana niandika ujumbe, kwani nilishabaini kuwa aliyelonga kwenye simu si kidume kweli ila nimefukuzwa kwa njia kupitia kidume mwenzangu tu kwa hofu kuwa mimi ni msema kweli kwa kumfanyia marekebisho kwani alikuwa na mwendo mgumu usiohatarisha,haya yote yanatokea baada ya hitilafu kubwa kati yetu lakini si hitilafu ya kuhatarisha bali ni itikadi za maisha kila mmoja anajiona yuko sawa zaidi ya mwingine,mitazamo iko kinyume nyume.

Nikaona mambo yanakwenada upogo sasa,nikatulia nikajihoji kwanini,nikasalimu amri nikaseama yote heri lakini nikachia ujumbe kama huu utambae kichwani mwake ..........."Praise of the Folly,shall forza companie".....daa sentensi kali sana hii na naipendamno na kuiamini na ikiwa andhani ni utoto mwanangu ameumia sana.Maana walijisifia kwamba wanapendana mno kumbe ni kiini macho...mara leo namba ninayopigiwa....mpigaji haongei...mara...niwekewe sauti ya zima moto mara..... lakini sijibu kitu.....yaani ni "dirty off you shoulder" ....ukurasa mwingine .....,,.,,..,,n.k

Hivi kwanini YASINTA umefanya hivyo?kwanini unachukulia maisha kama mbio za vijiti? maana mbio hizo ukichoka bora kujitoa kuliko kujifanya kinara huku uhai unatoweka.
bado kauli niliyoambiwa mwaka 2000 naikumbuka kwamba...."mwongoze mwanamke mkiwa barabarani.." yaani sikuelewa ila siku hizi nimebaini kumbe ni kujifanya unampenda sana msichana basi umkumbatie hadharani yaani popote...sijui kupigana mibusu......na nini...sijui barabarni...n.k .. hadharani nayo ni njema au vipi maana kijana sijui kitu waungwana,yaani siyajui hayo toto lililozoea kuvua samaki na kuogelea na watalii waliokuja ziwa nyasa enzi za mapadre wa kizungu(wa kikoloni) we aah acha tu.

Nilishasema kwamba ndugu yangu mimi ni mtu sahihi,lakini kazi bure wanapenda kuvinjari na maisha ya kwenye runinga za kimagharibi..lakini kijana sijui hayo si kwa ujinga bali msimamo,hoja n.k. Huyu binti ananifanya niwaze wasichana wote kama ni majeruhi wa maisha yaani hawana kile wanachoamini katika mahaba yao(samahani najua si wote).Yaani angejua sasa ninavyo watazama wasichana kwa jicho la pembeni nikiamini kuwa siku yoyote yatatokea kama ya WTC huko marekani,yaani nakimbia kama mbio za akina mzee Bayi.

Yaani naogopa kuelekeza mawazo haya na mtazamo wangu juu ya masuala haya tena basi bali ni kujibisha katika shughuli zangu ikiwemo kuandika porojo zangu katika anuani hii,bora kuliko kumtaka mtu ambaye haoni umuhimu wa kutakiwa na asiyemtaka.Hivi kwanini alifanya hivyo au wasichana wanapenda sana kubembelezwa? aaaaahhh hapa najua si hivyo ila nauliza tu.wala sijui kubembeleza ndio nini jamani...

Basi ndio hivyo nimeamua kuwa na maarifa mapya,mtazamo mpya,fikra mpya,mapinduzi mpya, sitaki kupoteza muda wa kuinua maisha yangu kama alivyotuasa 2PAC.Wasomaji niacheni nizungumze kama mwndawazimu maana huyu dada hajui kama mimi nilikuwa namhitaji sana na nadhani ipo siku atatambua kwamba aliyekuwa akimhitaji ni mimi,potelea mbali sasa nimefunga masikio nasaka fikra mpya kutoka sayari mpya na siyo dunia tena labda wasizaliwe na mwanzo wa HAWA na ADAMU.aaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhh...acheni nicheke...ooooooiiiiiih
Si mkwara bali akiona hapa aone kama sitanii kitu nimekuwa mwanaharakati wa mapinduzi ya kweli hakuna muda wa kuzubaa tena.

Pole kwa kunifuatlia sana lakini huyu binti naamini ninaweza kuonana naye muda wowote ila tatizo ni mitazano tu,yupo anajidai anakamua kitabu cha sheria za shahada huko.......na naamini kwamba ananiheshimu kama ninavyomheshimu kama wanadamu wengine.
kila la heri kwa maisha yake hayo....lakini kwanini alifanya hivyo?alidanganya kwamba aliyeongea nami katika simu ni waubani wake wakati naitambua sauti ile,hata hivyo mtu aliye karibu yake anashindwa kuniambia ukwEli kwa kuwa anajua sina muda wa kuujua UKWELI HUO TENA kwani nimeshaujua na sihitajiki kuujua zaidi bali.......

KWAHERI.......

1 comment:

  1. Jamani huyu binti ndio kwanza nafikiri amenipa hali ya kupambana upya na dunia.
    Nimepata ari nyingine ya kuinua maisha yangu...na huu ni mwanzo tu nitakusanya toka bara.....mpaka .....visiwani..
    tuombeane uzima,lakini kukusanya huko ni maaraifa na mtazamo mpya.

    ReplyDelete

Maoni yako