September 05, 2008

Harakati za Olimpiki....London 2012

Kama mlidhani ni dhihaka basi mlikosea sana, najua kaka Mbilinyi na dada Yasinta wataanza kucheka hadi meno yawaanguke. Hakika mtajiju leo,nawaambia harakati za olimpiki zimekwisha kuanza,yaani hapo ni saa 6 mchana jua lilikuwa kali lakini wapi bwana kazi tu. Unamuona huyo jamaa anayjifanya swala tano(natania) ni Bwana Thomas naye ni kichwa ambacho kinakwenda pale chuo kikuu Dodoma,yeye isyo swala tano bali manjonjo tu hapo kanipa maziwa kupozea makali. Yaani nawambia kama mwadhani utani ebu waleta hao Erick na Yasinta niwaonyeshe sughuli pevu. Sasa nimeanza kukimbia mita 10,000 baada ya kufanikiwa ile ya 5,000 na 3,000 lakini msiniulize muda niliotumia msije mkafa kwa kihoro na wivu ati kwakuwa nimempiku Bolt na Powell huku nikumkumbuka kipenzi changu Josiah Thungwane toka kwa mzee madiba mandela. Nimepumzika kidogo wiki hili kuvua samaki lakini nimebanika wengi mno njooni mle kama vya watu vinaliwa ...mtalipa

2 comments:

  1. hahahahahaah siamini kabisa kumpita Bolt itakuwa hadithi na kumpita Erik na Yasinta hiyo ndo itakuwa mbaya zaidi. Unajua sasa hovi nimeangalia golden league na Bolt amekimbikia mita 100 sekunder tisa point saba saba.

    ReplyDelete
  2. mjomba hayo maziwa hayakuwa matamu?

    ReplyDelete

Maoni yako