September 06, 2008

Olimpiki 2012 nyie chekeni tu...kazi ipo

Haya tena dadangu Yasinta kacheka sana niliposema maandalizi ya olimpiki nayaanza. unajua kwanini anacheka? ngoja nikumegee siri...aaah nimeghairi usije ukamwambia lakini sikiliza najua anawivu hawezi kukimbia mita 10000,pia 100 inamsumbua si umemuona alivyo? labda enzi zile akiwa kama Madonna mwaka 1992 angeliweza lakini sasa thubutu yake atajiju leo. Nakwambia sasa ni shughuli kwelikweli sitaki blah blah hapa wala mzaha. Najua hata Erick hawezi kuufikia moto huu yaani ni zaidi ya Usain Bolt yule jamaa anayetokea kule walikuwa wanahusudu sana BLACK BAMBOO eti sasa wanatingisha dunia kwa kukimbiza upepo. Asikwambie mtu yaani mpango wa kwanza kwenda kutambika mizimu kule BUTIAMA kwa Mwalimu JK Nyerere hakua kwere hapa. baada ya kutafuta pumzi sasa inatafutwa kasi. Ngoja nitakwambi nilitumi muda gani mita 10000 lakini mpaka nikaague kwanza kwa mganga ili nijue nitakimbia muda gani.....

2 comments:

  1. sasa ndo nimecheka zaidi mpaka nimelia. Watu bwana et Yasinta hawazi kuki mbia 10000 wala 100 et labda ingekuwa mwaka 1992. Kwa nini watu wana dharau hivi we subiri huo mwa 2012 au kwa nini tusubiri mpaka kwote huko. mwakani nakuja Tz halafu wewe,mimi na Erik tufanya mazoezi halafu utaona kazi yetu

    ReplyDelete
  2. pole sana kama ndo unamtegemea mganga hautafika mbali kwa nini kutumia mganga kama kweli una uwezo wa kukimbia afadhali waachia hiyo nafasi wengine. POLE sana kwa kutegemea mganga ngoja niwafahamishe Yasinta na Erik wasidhulike. mmh watu jamani

    ReplyDelete

Maoni yako