September 26, 2008

kwa wanaotaka kwenda majuu - II

Awali nilikuwa sielewi kwanini hawa watu wangu wanataka kuondoka nchini mwetu, lakini baadaye nilipokuwa Uchina na bwana Mao rais wa pale nilielewa sababu zao kwani nilikutana nao wataalamu wetu walioondoka Tanzania. Walinieleza sababu zao zenye maana kabisa,nikaelewa kwamba wanamipango mizuri. ...hata hivyo nikawaambia msisahau nyumbani jamani si mnajua kule mmewaacha ndugu zenu. kumbukeni hata sisi tulisomeshwa na mkoloni halafu tukapambana naye kwahiyo hata ninyi mnaweza kupambana nami kama sifanyi yale yanayowapendeza,huo ni utumiaji wa elimu. Sasa mkiondoka hawa wasiojua kitu watapambana vipi,watanitikisa vipi wakati siwaogopi. Lakini vijana wetu wakifundishwa kwenda mahala bila mipango,kuondoka kinyemela kwa ahadi za watu wasiowajua wala utamaduni wao,nadhani taifa litaaibika sana. Mnamwachia Mwl.NYERERE kupamba na umasikini kwani yeye ndiye aliwaletea? Haaa(kicheko). Lakini ninyi watu lazima mfikiri siyo kuhubiri tu maghorofa ya ulaya na amerika hapa..hayakuja bure shauri yenu....na...na ....na elimu yenu bado mnawapatia kila jambo hawa ndugu zetu...(wazungu).Msidhani kwamba mnyasa ninaandika mambo gani..kwani naona ile kasi ya kutaka kuishi majuu kwa kusingizia kusoma na wengine kutafuta kazi imezidi sana.Wabongo hayo maneno ni ya huyu mzee pichani JULIUS KAMBARAGE NYERERE.kama siku ya mwisho kuwepo duniani ningelikuwa naye,ningelimuomba kichwa chake yaani ubongo wake tu basi. Lakini kama kweli tunadhani elimu bora iko huko ughaibuni,elimu yetu airekebishe nani? tukisha soma huko basi tunaomba kazi hukohuko tena kufagia n.k baada ya hapo unarudi bongo unalalamika mbona hali haibadiliki? eboo! huna adabu akubadilishie nani wakati ulipomaliza shule hukurudi kuibadilisha si ulikwenda kuishi na yule Mwenyekiti wa Marais waongo duniani Joji Kichaka? Natumia lugha kali bila kutumia tafsida ili mpate ghadhabu na kuongeza juhudi. Mungu akupe hekima Ndesanjo Macha, Fred Macha nipo nanyi daima.Jikomboe. Uhuru daima

4 comments:

  1. Ngoja niwaambie wote waliokuwa ughaibuni tufanye haraka na turudi kwetu Afrika kwani naona watu wanakasirika kweli mpaka mimi naogopa. mmh ngoja nirudi Afrika bwana

    ReplyDelete
  2. ndugu yangu siyo kukasirika hapa bali ni kuwaonya wale wenye kutokwa na udenda/udelele/tamaa/hamu za kwenda ughaibuni. hawa jamaa wanakwenda wafikiri huko kuna maisha ya kwenda kuazima nguo za washkaji kuvaa. wanadhani kuna wale tu wenye maisha mazuri. halafu wamesahau zile zama za QUEENS au maerican Welfare kwa watu weusi kwamba walikuwa wanasaidiwa na serikali. poa lakini huku kwetu hakuna hiyo tena unaweza kwenda kuzengea/kuvizia/kudowea msosi kwa jiarani. nyooooooooo ughaibuni utaodowea kwa nani. jamani someni sana maandiko ya Fred Macha, tena kaandika mfululizo makala tatu sababu ya mbongo mmoja kumbeza mzee Macha na kumrundikia kejeli kibao bila kuelewa analofanya...lakini mwisho wa siku anadoda hapahapa bongo. hii tabia ya kulalamikalalamika hii we ngoja tu. Sitaki kuishi na Joji Kichaka mwenyekiti wa Marais waongo na mwizi wa kura kule Texas

    ReplyDelete
  3. Nimefurahishwa napicha na maelezo hayo kwa mwalimu wetu Nyerere daima zidumu fukra zake.

    ReplyDelete

Maoni yako