September 25, 2008

makosa+urafiki+kumbukumbu+msamaha


Ngoja niandike kwanza leo. Yasinta Ngonyani ni dada yangu,rafiki yangu na mtu wangu wa karibu.Lakini katika kipindi chote hiki nadhani mnaelewa watu wakiwa marafiki wema hushauriana kupiga gumzo na mseto wa michapo n.k. Nimeamua kuandika kwasababu najua nilimkosea rafiki yangu mnyasa mwenzangu,mngoni mwenzangu,mtanzania n.k hata hivyo nadhani hakuna matata. Ila nasema kweli dada Yasinta nimeamua kuandika hapa ingawa najua utaniuliza busara zangu kwani yalikuwa masuala ya kirafiki na binafsi zaidi,lakini ujue mwenzio wala hata moyo hauridhiki najihisi kukosea. Kwahiyo naomba nisamehe 7mara 777. nafikiri unajua kwamba utasema hakuna kosa lakini nakupenda sana dadangu nikikosea nisahihishe mdogo wako mimi kwani naamini una mengi uliyoyaona kukukuta. Kwani historia yako inanipa uchungu inanikumbusha namna ambavyo sijafaidi raha za wazazi sababu ya shule yaani tangu darasa la sita nipo mbali na wazazi kwahiyo wakati mwingine naona siitendei haki nafsi yangu. Salamu kwa shemeji,mjomba wangu Eric na Camilla waambie msameheni anayejuta. Unajua kwamba kuna wakati sitendi kama ninavyopaswa lakini nashukuru kama unaelewa kwamba mdogo wako nipo katika hali gani. idumu blogu ya ruhuwiko. Amina

3 comments:

  1. Mhh hapo ndugu yangu ipo kazi kwani inaonekana huyo dada Yasinta ni mtu muhimu sana kwako. Je umejaribu kuongea naye, au yeye anajua ni kosa gani umemtendea. Mmeongea au haiwezekani hata kuongea, Ni udada tu au kuna historia nyingine kwani katika picha anaonekana ni mtu mwema na wa kusamehe kwa haraka. Kama kweli una kosa basi itakuwa kosa kubwa sana. Jaribu tena kuongea naye atakusamehe tu na mtakuwa marafiki, dada na mdogo/kaka kama ilivyokuwa zamani. Nakutakia mafanikio mema

    ReplyDelete
  2. mmmm mwenzangu labda nimechanganyikiwa kwani sasa kuna maswali makini sana katika maoni yako. uanajua kwanza siwasiliani naye sana kama zamani yaani ilikuwa kila mara sms haziishi n. lakini nikawa kama mbishi halafu mwenzangu anatumia muda kunitumia ujumbe mi nadengua naringa yote tisa wakati anapiga simu basi hakujibizana vizuri,nikaona ametamka neno 'aaaaaaaaahhhhhhhh' ile kwa jazba nadhani unajua. nikajua habari ndiyo hiyo kwani nimeharibu. unajua nampenda dadangu kwani wahenga walisema kwamba iwapo unataka utendewe meme ni lazima nawe uwatendee watu kama unavyotaka kutendewa. ukisema ni mtu muhimu sana unakosea. ngoja nikueleze falsafa na itikadi zangu ni kwamba kila mtu hapa duniani kwangu ni muhimu sana kwani naamini katika falsafa kwamba tupo kwa ajili ya wengine. kwahiyo hakuna amjuaye mtu muhimu katika ulimwengu huu kwani unaweza kusaidiwa au kujikuta unakuwa na watu ambao hukutegemea kama wangelikuwa muhimu kwako-labda nijaribu kunyamaza kama nilivyo tabia yangu. mmm labda nilichanganyikiwa kwani kosa langu lipi vile? nikumbushe nimesahau

    ReplyDelete
  3. sasa wewe mbona unanichekesha sana kama wewe hujii kosa gani kwa nini unamwomba dadako samahani. Je? huyo dadako inavyoonekana amekasirika? Basi muulize yeye ni kitu gani kimetokea mimi siwezi kukusaidia kwani si shahidi wa jambo hili. Ni kweli kabisa mtendee akutendeaye. umemwambia dadako kwa nini ulikuwa unadengua/ringa.

    ReplyDelete

Maoni yako