December 01, 2008

mauzo ya kondomu

Mara nyingi napenda habari mpya zenye vituko ambavyo vinanipa kazi ya kutafakari lakini sipendi vituko au habari za kunichosha ingawa sichoki mwili akili inagota.

SASA: Mauzo ya Kondomu huko Korea yamepnda sana tokana na watu hususani vijana wadogo kujihusisha na utamu wa ngoma ya kikubwa NGONO. Mauzo hayo ni kwa mujibuwa Dk Janet Hyde aliyefanya utafiti katika jamii za watu wa Korea toka chuo kikuu cha Wiscons. Anasema wingi wa Runinga, pamoja na mhusiano mabaya ya wazazi majumbani ni mambo ambayo yanaaminika kuchochea vitendo vya ngono kwa vijana wa umri mdogo.

Wengi wanaangalia vipindi ambavyo vinaashiria au kupandisha mzuka kama siyo midadi ya ngono na hawavai kondomu. Lakini hivi karibuni utafiti unaonyesha kondomu inanunuliwa sana tu ili kujiburudisha na majambozi ya kiutamu utamu!!!! Vijan wengi ni wale wadogo wenye umri wa miaka 13 na 15 ambao anadai wameshafanya ngono kama siyo kufaidi utamu huo katika umri mdogo. Mauzo yameongezeka sana kipindi hiki kuliko ilivyokuwa awali:Na maadili yamekuwa mabaya sana siku hzi huko KOREA

HIVI ndivyo vituko, lakini nafikiri unaweza kuwaza jambo. JE JAMII ZA KITANZANIA ZIPO VIPI? VIPI WALE WAPUMBAVU WANAODAI UTANDAWAZI huku hawana lolote katika utandawazi wenyewe? Je utandawazi hauna maadili? PAMOJA DAIMA!!!!!!

7 comments:

  1. jamii yetu ya kitanzania tupo wapi kama Taifa?

    ReplyDelete
  2. Tanzania siku hizi wameadaputi sana mila za majuu utawakuta nao suiku ukitaka kufanya utafiti juu ya kondomu hapa nchini utabaini zinanunuliwa sana hasa mjini.

    ReplyDelete
  3. Kuna wakati fulani nilipokuwa nafanya kazi katika asasi inayotoa elimu ya afya, nilipata bahati kushiriki utafiti mmoja. Tuligundua kuwa maendeleo ya teknolojia yameleta mambo katika jamii zetu.
    Vijana wengi wanapata hamasa katika intaneti, katika filamu, katika video za muziki na katika majarida na magazeti. Na hii teknolojia ya bluetooth, ukichunguza simu za vijana wengi, zimejaa picha za ngono. Vitu hivyo vimeleta msukumo mkubwa, vimewafanya vijana kuwaka tamaa.
    Hivyo manunuzi ya kondomu lazima yataongezeka. Hili jambo halitokei huko pekee, halitokei Tanzania pekee, linatokea dunia nzima.
    Wanasema maendeleo huja na mamboleo.
    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  4. Kwani maendeleo ni nini? Ama tunaposema tumeendelea tunakuwa tumemaanisha nini? Kwangu mimi kila aina ya mabadiliko ni maendeleo ila swali linabaki kuwa ni MAENDELEO KUELEKEA MAFANIKIO AMA MAANGUKO? Ni kweli kuwa ili uamke watakiwa uwe chini lakini ukiwa chini utakuwa mahala utakapoweza kuamka? Yaani kuna kulala na kufa na tukichanganya haya tutakuwa tunakosa ukweli. Yeah Maendeleo yanakuja na madidimio yake na pia kila fanikio la mmoja ni kushindwa kwa mwingine. Manunuzi ya Kondomu yakiongezeka sambamba na maambukizi sijui tunakuwa tunafanya nini. Ukweli utabaki kuwa tunawanufaisha watengenezao Kondom na dawa za waathirika huku tukiua nguvu kazi na jamii yetu.
    Ni CHANGAMOTO YETU sote kuamka na kuwaza vema juu ya haya.
    Blessings

    ReplyDelete
  5. wakuu mnatoa safi sana, sijui Dada Yasinta yuko wapi??? au hii mada imempiga chenga na kaka Simon, aaahhh najua kwakuwa hakuna BIA hapa au? maana nawaona sana wakichangia hawaachi BIA.

    ReplyDelete
  6. Mi nipo. Ni hivi hizo kondom. Ni kweli maendeleo kuwa kila sehemu kondomu zinauzwa au zinagawiwa kwa watu lakini je? kuna elimu yoyote inatolewa kuhusu kondomu kwa vijana? kwani inawezekana wengi wananunua na hawajui matumizi yako hasa huku kwetu kijijini.

    Je? hizo BIA zipo sasa?

    ReplyDelete
  7. Ah jamani asanteni PAMOJA DAIMA.lakini matumizi ya kiswahili jamani muhimu sana au vipi mwanawane, kiswahili safi bila kuchanganya aaah lakini ni uhuru wako? KONDOM za nini jama???? utamu utamu mpka kisogoni halafu mnasema kondom, ebu mniambie nimetoka zangu kuvua Mang'ong'o au kambale nimechoka ninakotoka mbali kilindini huko, halafu nikija nyumbani namwambia Mamsapu tujifumanie wenyewe eti nitumie kondom?? au nimetoka zangu kilabuni na MAHIVI halafu nakupa Kamwali njiani ninunue kondom?? mwe hamjui mambo yote haraka haraka.
    HIVI inafikirisha mawazo yangu? nasimama kwa niaba ya watu gani, unanielewa? KONDOM ZA KIKE ? mnalelewa? sijui labda nimetingwa kidogo

    ReplyDelete

Maoni yako