December 29, 2008

nini msingi wa IMANI?

Nilidhani sitoweza kublogu karibuni sababu ya HAMU ya kumngoja dadangu Yasinta, lakini naona kama nilivyosema kwamba blogu ni kitulizo cha moyo wangu. Najua dada Yasinta akija mambo poa.

LAKINI
Baada ya kusoma mambo kadhaa kuhusu imani zetu, nimeona niwasilishe swali katika kijiwe chetu cha MASWALI MAGUMU- Yasinta, Bwaya, Mzee wa changamoto, Simon,Kaluse,Fadhy, Fita,Mzee wa taratibu,Kalama,Markus na sasa dada Koero.
Swali hili linatokana na hoja za dada Koero Mkundi kwamba biblia ilikosewa na maoni yake kuwa hakulenga kuuponda ukristo, sawa nakubali! hasa baada ya mimi kuhoji mantiki ya injili kadhaa kuachwa ikiwemo ya 'bikira' maria.

LABDA
nilikosea kuhoji lakini nimefurahi sasa dada Koero kutukumbusha mambo kadhaa kuhusu imani. Mimi naona tujadili hili suala kwani hata kama tunajiona tunapoteza muda lakini lazima tujadili, lazima tujiulize kuhusu imani hizi za mashariki ya kati.

Swali lenyewe.
Je unaweza kuikana NAFSI yako katika mwenendo wako wa maisha?
Je unaweza kukubali kwamba unaongozwa na IMANI ya dini kuliko IMANI yako katika nafsi yako?
Je kwanini walisema uikane nafsi yako?
Je iwapo tunaamini kuwa kilichoandikwa ndicho, mbona kuna utamaduni wa maeneo yao husika?
Je tunaongozwa maisha yetu kwa IMANI ipi?
Je twaenenda kwa IMANI au kwa kuona?
Je nafsi zetu hazina imani thabiti?

BASI unajua nilitaka tu kijiwe cha MASWALI MAGUMU tujumuike kufundishana haya mambo hasa mimi nisiyejua kitu kwani nimekulia na kulelewa na wamisionari na kuwa na ndoto ya upadre LAKINI ikayeyuka. kwanini? kuusaka ukweli? Labda waafrika hawakuwa na IMANI ndiyo maana twaenenda kutoka mashariki ya kati.
mmmm labda nimechanganykiwa kidogo au?

5 comments:

  1. Ntarejea. Wacha nilishe minyoo na kutafakari.
    Asante

    ReplyDelete
  2. habari Mkuu, leo nimepita hapa kijiweni kwako nikakutana na hii mada.
    Naomba unipe muda nikutafutie majibu.

    ReplyDelete
  3. Habari kaka Mpangala,
    Nimepita hapa kutoa shukrani zangu kwako kwa kunikaribisha Nyasa.
    Nakushukuru sana kwa kunitembelea, na kuchangia mawili matatu katika blog yangu.
    Ahsante sana.

    ReplyDelete
  4. Mambo kaka? Nami nimepita kama wenzangu. Sijapita siku kiasi.
    Ahsante kwani kazi zako bado zimesimama vema.
    Kuhusu imani kaka, ngoja nikajiulize kwanza kwa mwalimu wangu wa mafundisho ya kipaimara.
    Hivi, ok, nakutakia mwisho mwema wa mwaka na mwanzo mzuri wenye neema wa mwaka mwingine.
    Kama kaka Mubelwa apendavyo kumalizia, Blessings!

    ReplyDelete
  5. Waungwana nanyi nawaombea mema msitie shaka.

    ReplyDelete

Maoni yako