December 31, 2008

Wanaopuuza shauri yao


nimesoma maoni ya Koero katika shajara/blogu ya Bwaya kuwa wapo wanaotazama blogu kama upuuzi. Nimefarijika kuona dada Koero kawagundua watu hawa lakini anawashangaa wanasoma mambo ambayo wanasema ni upuuzi. Namshukuru kwa kuwabaini LAKINI naomba uwaaambie blogu siyo upepo wa kupita, hii ni hatu nyingine zaidi ya kusoma magazeti na kuangalia luninga. Hapa hatuhitaji wahariri wakuu wala waandamizi bali nidhamu imejenngwa na mtu mwenyee. Kwa hakika watu tunajikuta tunafanya mambo ya ajabu lakini kujipa muda angalau kufanya jambo linalokufanya uwe bize na kuepusha porojo za hovyo LAKINI watu wengine hawaelewi. Jamani nia yangu ni kwamba pamoja na kwamba wanasema ni upuuzi ambao wanausoma lakini wajue kuwa blogu siyo upepo. Nashukuru dada Koero amegundua hilo maana kuna watu ukiwaeleza hili jambo wanaona kama ujinga fulani, eeeeh shauri yao wanaopuuza tunajua hawaamini kuwa wasomaji wanaweza kuwa wahariri na wahariri wanaweza kuwa wasomaji. Hivi huamini tunaishi zama zingine za teknolojia? Wape maneno yao dada Koero asante kwa kutukumbusha wanaopuuzia blogu/shajara shauri yao.

5 comments:

  1. hapa ipo kazi kweli kweli alama mpaka kichwani mmmh! haya mi naacha nimeshindwa

    ReplyDelete
  2. Nawatakieni heri ya Mwaka Mpya bloggers wote.
    Na wasomaji wetu.
    One love.

    ReplyDelete
  3. Habari kaka Mpangala.

    Nakutakia heri ya mwaka mpya wa 2009.
    Naomba tuendelee kushirikiana kama mwaka uliopita.

    ReplyDelete
  4. Asanteni nyoteeeeee nami nawatakia mafanikio mema na tushirikiane kama ilivyoada

    ReplyDelete
  5. Nimefurahi umemushauri vizuri dada Koero ni kweli kabisa ya kwamba wanaopuuza blogu watajiju hwatajikuta wanabaki na mambo ya zamani.

    ReplyDelete

Maoni yako