January 10, 2009

Aggregators+Bloglines =vikusanya habari

AGGREGATORS: ni moya teknolojia tunazoziita teknolojia za kutunza muda. Vikusanya habari vinatunza muda kwa kutuwezesha kujua BLOGU zipi zimeandika habari mpya/mambo mapya badala ya kuzitembelea BLOGU moja moja. Inawezekana pia ukatumia vikusanya habari kupata habari toka katika tovuti mbalimbali za habari na siyo BLOGU pekee.
Huduma ya AGGREGATORS ni kama huduma ya BLOGLINES, inachofanya ni kukusanya habari toka kwenye blogu mbalimbali unazozipenda na kuzileta katika ukurasa mmoja.
KAWAIDA; ukitaka kusoma blogu upendeleayo unachofanya ni kuzitembelea kwa kuandika anuani zake.
Lakini unaweza kutembelea blogu 10 halafu hazina habari mpya. Sasa hii BLOGLINES inakuletea mambo mapya yaliyoandikwa katika blogu uzipendazo. Fungua blogu yako ingia halafu bonyeza LAYOUT ili kuongeza ukurasa mwingine uupendao. Utaona orodha ya kurasa ambazo ungependa ziwepo, ndipo utakuta BLOGLIST bonyeza halafu utaona neno ADD kisha andika blogu unayoipenda kusoma habari zake. Sasa hapo kichwa cha habari kimeandikwa MY BLOGLIST unaweza kubadili kama ambavyo nimefanya, mfano: mimi nimeandika kikusanya habari(tazama kulia kwa blogu yangu).
Unaweza pia kusoma hapa; www.mwongozo.wordpress.com
NB ukiwa na tatizo, ni vema tukatafutana ukipenda, napatikana Sinza Kijweni ofisi za New Habari house siku za jumamosi ni poa sana

3 comments:

  1. Hili darasa nilikuwa nalisubiri kwa hamu, hii ndiyo faida ya kufahamiana na wasomi, (Sorry dada Koero kasema kuwa hakuna wasomi)
    Hii ndio faida ya kufahamiana na Markus Mpangala.
    Mzee nitajaribu nikishindwa nitakuja kukuona hapo ofisini kwako.
    Nitafanya miadi kupitia humu humu blogini.
    Ukitaka kunisaidia zaidi ni SMS kwa namba hii ili niweze kukupata kirahisi zaidi. 0715 729292.

    Ahsante sana kwa darasa murua.

    ReplyDelete
  2. Usijali sana kaka Kaluse, tupo pamoja, nita ku-SMS bila matata au vipi. huduma poa sana hii yaani inaondoa ile dhana ya kuweka orodha ya blo nyingi halafu ukifungua hazina habari mpya. nadhani jumamosi nitaku-SMS

    ReplyDelete

Maoni yako