May 21, 2009

Kikao cha Dharura kuhusu NYASA

nilipotea kidogo, lakini nilikabiliwa na kikao kizito na muhimu zaidi kuhusu NYASA. Nambukuka mwanzoni mwa mwaka huu mzee wangu Profesa Joseph L.Mbele alinishauri kuhusu kuandika kitabu kuhusu nyasa. Nililipokea wazo lake kwa mikono miwili huku rafiki yangu koero akisisitiza jambo hilo.

Hata hivyo naweka wazi kwasasa kuna kikao kizito kuhusu nyasa, kikao ambacho kinaendeshwa na wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wametoka katika ukanda wa nyasa. Kikao hicho kinazungumziaq maendeleo ya maeneo hayo na namna ya kuanzisha umoja ambao utawezesha jamii za nyasa kielimu,siasa, na uchumi. Jambo hili nashukuru linafanyika huku wazo la mzee Mbele likiwa mezani kwangu.

Jumapili iliyopita kulikuwa na kikao hicho, tulijaribu kuweka ama kuorodhesha kero na mambo mazuri ambayo nyasa tunayo na tunaweza kuwafaidisha wakazi wake. kikao hicho naweza kukiita NYASA DEVELOPMENT ORGANISATION. ni wazo ambalo tumeamua kwa moyo mmoja kujitolea kwa kuanzisha kikundi hiki kwa nia ya kuendeleza wananchi wa amaeneo yetu.

Kikao hiki cha kwanza kimefanyika huku wahudhuriaji wake ni BARAKA WANDAWANDA, HELLEN LOCHI. LAWRENCE EMANUEL, BONIFACE MNDALA, EMMANUEL NAMINGA, RICHARD MWANJA, VENANT KATOPOLANGA, SIMON HARRISON, FRANK NDOMBA, FRANK MAPUNDA, na LIBADA MAPUNDA pamoja na MARKUS HONORIUD MPANGALA.

Sisi siyo mwsho bali wenzetu wengine walikabiliwa na majukumu ya chuo, kwahiyo tunaamini kikao kijacho cha jumapili wiki hii kitakwenda katika mpangalio uleule. jitihada ni kubwa na ari yetu ni kubwa sana kwani kikundi hiki kinaundwa na vijana ambao wastani wa umri wetu ni chini ya 25. Tumedhamiria na tunahakika lengo letu litafanikiwa.

Mipango yetu ikiwa katika njia sahihi nitawahabarisha zaidi ili mjue dhamira yetu watoto wa kinyasa kuwa tunataka kufanya nini katika ukanda wetu na watu wetu. Kundi hili linakaribisha mwanachama yeyote ambaye anaweza kukiboresha na kusaidia mambo mbalimbali hususan mchango wa mawazo ambao ni muhimu sana. Vilevile ingawa ni suala binafsi sana lakini nawaomba Raiton Mbele(Ukraine), Robert Ngalomba(UK) na mzee wangu Mbele kuwa mchango wenu ni muhimu sana. Yasinta Ngonyani(sweden) nawe pia tunaamini kuwa upo pamoja nasi. Pia Mzee wangu Prof Mbele ningependa na nitakupendekeza uwe mlezi wetu iwapo nafasi itakuruhusu kwani mchango wako ni muhimu sana. Jumapili iyajo(juma hili) tunakikao cha pili ili kufikia maazimio yetu.
Tunakaribisha kila ya aina ya mawazo yenu wanablogu wote bila kujali ukanda wala mahali ulipotolea bali tunachofanya ni kujaribu kuwezesha jamii zetu. Sasa ninajikita katika kujitolea kwa jamii rasmi bila malipo. Tunawakaribisha sana nyasa.

2 comments:

  1. Natoa pongezi kwa uamuzi huu na naunga mkono. Tutakuwa bega kwa bega.

    ReplyDelete
  2. Napenda kutoa pongezi kwa wale wote waliopendekeza kuanzishwa kwa kikundi hiki,na wale wote wanaohudhuria vikao mbalimbali na kutoa mapendekezo ili kuleta usanisi wa kikundi hiki.Napenda kuunga mkono na kuahidi tutakuwa pamoja kuhakikisha kikundi hiki kinafanikiwa malengo yake.MUNGU awabariki wote wanaounga mkono kuwepo kwa kikundi hiki.

    ReplyDelete

Maoni yako