June 02, 2009

KUSOMA> Mkononi ninaye YASSER ARAFAT

Pamoja na harakati au mchakamchaka wa maisha na shule kunibana kwa mitihani miiiiiiiiingiiiiii, lakini sijaweka kando jambo hili. Ninaye mkononi Yasser Arafat nakula nondo zake, najielimisha. Lakini bado kitabu cha Prof Mbele ninahamu nacho sana tena sana.
Sasa nadhani mambo ya mzee wangu Freddy Macha na semina za ujuzi zimekwisha, nimefaidika nimejifunza, tunmeongea mengi, tukafurahi na kupiga gumzo la hapa na pale. Vilevile mkononi ninaye TOM CLANCY katika THE CARDINAL OF THE KREMLIN. haya msije mkasema nimeacha kuvua samaki na kuvamia kusoma. Mimi na samaki ni kama mizizi na ardhi. KOERO mwana wa MKUNDI upo hai au umekumbwa na KIDELI maana siku hizi duuuh! haya mambo ya aiseh! ha ha ha ha

1 comment:

  1. Shukrani kwa kunikumbuka. Nafurahi kusikia ulihudhuria semina za Freddy Macha. Freddy anatoa mchango mkubwa kwa Taifa na kwa ulimwengu kwa ujumla. Ni balozi mahiri huku ughaibuni, kwa njia ya muziki na uandishi wake. Pamoja na kuwa anaaandika kwenye magazeti ya Tanzania na amechapisha vitabu vyake hapo, nafurahi alivyoweza kuja yeye mwenyewe kuonana nanyi ana kwa ana na kuelimishana. Nimeona taarifa na picha kwenye blogu mbili tatu.

    Kuhusu vitabu vyangu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, na Matengo Folktales, vinapatikana hapa Sinza, maeneo ya Lion, simu namba 0717 413 073 au 0754 888 647. Kingine, "Notes on Achebe's Things Fall Apart," kinapatikana Tanzania Publishing House.

    ReplyDelete

Maoni yako