June 18, 2009

Nani anapenda KISWAHILI chenu kichafu???

Kila nikipitia mitandao au kusoma magazeti nakutana na matumizi mabaya ya kiswahili, wengi tunatumia kiswahili vibaya, mtamshi mabaya, silabi mbovu, kanuni za lugha zimetupwa yaani kila kitu ovyoovyo tu.
Sina hakika kwanini jamo hili linasingiziwa kwa njia ya teknolojia lakini nidhahiri utandawazi ni nguvu ya utamaduni mwingine kwahiyoiwapo nchi inakuwa kama kundi la magabachori wale wasiojali hali za wengine na kukumbatia hali zao hata kama mbovu basi mambo ni juu ya mambo kuwa mabaya.

Yaani neno AAMINI= wanamaanisha HAAMINI
AMNA= wanamaanisha HAMNA
KUWA NA KUA= linatumika vibaya kwa kudhani ni maana moja
LISAA NA MASAA= wanamaanisha SAA
UJUI wanamaanisha HUJUI
UO wanamaanisha HUO.
ALAFU wanaamisha HALAFU

Nani kasema huo ndiyo ukweli wa lugha yetu adhimu? Kiswahili gani kibovu namna hii halafu mnasingizia zama mpya? Natamani kumezwa na ardhi yeoteee inifunike ili nikose kuyaona lakini natamani kuendelea kuishi. Badilikeni lugha iwe katika mhimili wake

No comments:

Post a Comment

Maoni yako