August 06, 2009

Toleo lijalo la CHACHAGE S. CHACHAGE?


Naam ni rafiki zangu, darasa langu, watu wangu kibingwa! Kutoka kushoto kweda kulia ni mtu wa nne, anaitwa STAN. Nimeandika kifupi tu ili ujue jila lake, ni rafiki yangu, kipenzi changu. Sikuo zote anaamini atakuwa Profes Chachage S. Chachage, nina hakika wewngi tunamfahamu sana kwa kazi zake tangu ALMASI ZA BANDIA hadi MAKUADI WA SOKO HURIA. Ngoja niwaibie habari basi, tayari kitabu chake kingine kinaandiliwa kinapikwa jikoni kwa wachapaji wa E nad D VISION PUBLISHING LTD, unajua kinaitwaje? ni hivi CHACHAGE, UCHAMBUZI WA SERA, UONGOZI NA MASLAHI YA WATANZANIA.
Ningeweza kuorodhesha vitabu vingi vya kampuni hiyo vijavyo ambavyo binafsi navisubiri sana hasa huyu Chachage. Basi rafiki yangu STAN ana matumaini hayo. na hao wote ni nondo kutoka chuko kikuu cha DSM. Au unaonaje msomaji wangu, unabisha kuwa hakuna Chachage mwingine ajaye? haya weee subiri mwenyewe halafu utaniuliza mbeleni.

2 comments:

Maoni yako