August 23, 2010

LITEMBO

Nilifika hapo nikiwa mdogo enzi zile za homa ya Pumu. Lakini amini nakwambia nilipona kwa dawa za Mitishamba, na kwa urahisi iliyochanganywa na Asali. Hakika nawashukuru madaktari enzi zile, lakini sasa sina dalili za kahoma hako. niko CADANGA kama Hugo Chavez pale Venezuela, yaani NGANGARI

3 comments:

  1. Yaani ungelikumbuka `combination' ya hiyo dawa, ungeshaukwaa utajiri hapa Dar,

    ReplyDelete
  2. Litembo enzi zile ilikuwa ni hospital maarufu sana. Umenikumbusha babu yangu mzaa mama alikuwa mgonjwa na alikuwa hospital ya litembo kwa muda mrefu alikuwa na upungufu wa damu. 1980 babu yangu mpendwa aliitwa na baba yetu wa mbinguni. Amina.

    ReplyDelete
  3. Hapo ndipo nilipozaliwa. Nilibatizwa katika kanisa linaloonekana hapo pichani, nikasoma darasa la kwanza hadi la nne hapo hapo. Nilitembea sana njia hizi zinazoonekana katikati ya picha, na kule mbali naona vijiji kama Mhindo, Mapelele na Mhagawa. Shukrani kwa picha hii.

    ReplyDelete

Maoni yako