May 25, 2011

KOERO U MZIMA, HONGERA SIKU YA KUZALIWA

Ni asubuhi na mapema, baada ya kujiweka sawa kwa kutoa jasho kidogo naamua kukaa kwenye kompyuta.
Huku nikiwa bado nahema kutokana na na kuweka afya vema ili kuanza siku.
Baada ya hapo najipa dakika ya kuipa upendeleo blog ya  VUKANI kwasababu nilijua ndiyo siku ya Koero Binti Mkundi kuzaliwa, nilitaka kuona ametuletea tunu  gani.
Hata hivyo nilichokiona baada ya kusoma nilibaki na simanzi. Uvumilivu ukanishinda machozi yakanilenga, mwili ukasawajika. Harara ya kuwasiliana na wadau wa VUKANI ikaanza.
Na kwakuwa nilikuwa kasi mno kuwahi majukumu, nikamuomba kaka Kaluse yapata saa moja hiyo asubuhi asome Blog ya VUKANI.
Nikamweleza na mtani wangu Fadhy, asome VUKANI.  Nilipokuwa naandika maoni, ghafla Waziri Ngeleja na Tanesco wakachukua umeme wao, ikabidi nisubiri mgawo.
Nikiwa naelekea kwenye majukumu, yapata saa mbili na dakika 29 asubuhi mtani wangu Fadhy alinijulisha atasoma VUKANI aone kuna nini.
Lakini nikamwomba anipe mawasiliano ya ya simu binti Mkundi kwakuwa namba niliyonayo kwa kweli inaninyima raha, simpati Koero.
Mtani wangu Fadhy akasema hana. Yapata saa 6 na dakika 10 mchana, Kaka Kaluse ananijulisha, “Nimesoma kaka. Imenigusa sana”.
Hakika Koero alinigusa hata mimi sio Kaluse peke yake, na Mtani wangu Fadhy. Nilijua Dada yangu kipenzi Yasinta atasoma mapema tu.
>>>
Koero u mzima,
Tatizo hakuna,
Ni shida ndogo,
Wala isikupe kihoro,
Mwaka 2009 mimi,
Mshituko nilipata,
Daktari akasema,
Markus dar haikufai,
Hukuugua masikio,
Leo yamekusibu,
Kubali hilo,
Nikasema si tatizo,
Bali uwezo umepungua,
Wala sihitaji kifaa,
Kwani naweza kuwasiliana vema,
Ila kuna wakati yanauma,
Yanapunguza uwezo kusikia,
Kama homa ya vipindi,
Nimeshazoea mimi.
Koero ijali afya,
najua umekubali hali,
Hadi leo umetuambia,
Imenigusa mno,
Imewagusa wengi hapa.
Mzee wa Lundunyasa anasema,
Koero tuko pamoja kwa shida na raha.
Tena umekuwa sehemu ya furaha ya wanablog,
Hongera mzee Mkundi
Kutuletea binti Mjuzi,
Mwenye vipaji pomoni.

3 comments:

  1. Hongera kwa siku yako Koero. kwa ujasiri na kuwa muwazi kitu ambacho katika maisha yangu nakipenda sana. Ahsante nawe Markus.

    ReplyDelete
  2. Greetings from Finland. Thus, through a blog is a great get to know other countries and their people, nature and culture. Come take a look Teuvo images and blog to tell all your friends that your country flag will stand up to my collection of flag higher. Sincerely, Teuvo Vehkalahti Finland

    ReplyDelete
  3. Mtoto mzuri kweli huyu Koero!

    ReplyDelete

Maoni yako