October 10, 2011

FREDDY MACHA NDANI YA DAR ES SALAAM+RATIBA YA WARSHA ZAKE

Freddy Macha akizungumza na waziri wa mambo ya nje Bernad Membe
Freddt Macha akiwa na wanafunzi wa sekondari ya Mwandege mkoani Pwani mwaka 2009. Sasa yuko nchini, fuatilia ratiba yake hapo chini.
WARSHA NA  FREDDY MACHA

Moja kwa moja toka London; mwanamuziki na mwandishi huyu Mtanzania atafanya semina ukumbi wa Fasdo, Tandika,  Dar es Salaam, Jumanne tarehe 11 na Jumatano  12, Oktoba, 2011.

Mwenyeji:
Fasdo:  (Faru Arts Development Organisation)
Mawasiliano : Chande Nabora: Simu 0713-310755
Nasibb: 0713-261011 

Mada

1.    Utafanikishaje afya yako? Chakula (kula sawasawa), mazoezi mbalimbali na mambo mengine kibao.

2.    Mtu anawezaje kutoka kwao kuishi ughaibuni na akafanikiwa? Mambo ya msingi unayohitaji kuelewa. Yalete maswali na mambo yanayokusumbua kuhusu suala hili.

3.    Je, unataka kuwa mwanamuziki?  Kwenu nyinyi wote wasanii wa leo na kesho, njooni mpokee vidokezo na ushauri.

4.    Je, unataka kuwa mwandishi msanii au mwanafasihi? Siri za kukufanya uwe bora zaidi ya wengine! Ongeza kipato chako kupitia uandishi wa kimataifa.

5.    Kukua na maendeleo ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza

6.    Ukumbi wa Maswali na Majibu

Mhusika

Freddy Macha ni mwalimu, mwandishi wa insha na habari, mwanafasihi, mtunzi wa vitabu, mkalimani, mwanamichezo, msingaji, mwanablogu na mwanamuziki.  Hapa Tanzania anajulikana zaidi kama mwanasafu, aliyeanzia kazi magazeti ya Uhuru na Mzalendo, 1976-1978;  akajenga jina na safu ya kila jumapili Cultural Images gazeti la Kiingereza, Sunday News 1981-84. Kuanzia 2003 amekuwa akiandika kolamu kadhaa nchini ikiwemo : Kalamu Toka London kila jumapili gazeti la Mwananchi na Chat from London gazeti la Kiingereza, The Citizen kila Ijumaa.
Anazo blogu kadhaa ; na hufanya kazi za usingaji, muziki, mtafiti na mtangazaji wa runinga mbalimbali za mtandaoni  mathalan Urban Pulse Creative Media na Global Fusion Music and Arts, Greenwich, London.

Baadhi ya kazi kuu alizozitoa:-
Ø  2006, kitabu cha Mpe Maneno Yake,  hadithi fupi fupi za Kiswahili alizokusanya miaka 30 katika nchi nyingi alizoishi na kuchapishwa na E & D Limited, Dar es Salaam.
Ø  2001,  Wimbo wa “Kilimanjaro” na bendi ya Kitoto, London.

Ø  2000, CD ya muziki na fasihi –Constipation- iliyotolewa na kusifiwa na majarida kadhaa Ulaya.

Ø  1996, hadithi yake “Nilipomuua Nyoka” (When I Killed a Snake) kwa Kiingereza ilichukua nafasi ya pili katika Tuzo la Jumuiya ya Madola, London. 
Ø  1995,  alitoa CD ya muziki na fasihi– Kitoto- Quebec, Canada.
Ø  1986 alichapisha mwenyewe mashairi  ya Kiingereza na Kijerumani (Papers! Papers! Papers! ) Cologne, Ujerumani.
Ø  1985, alichapisha kitabu cha maisha ya mwanamuziki Remmy Ongala.
Ø  1984, mkusanyiko wake wa hadithi fupi za Kiswahili : Twenzetu Ulaya (Gap, Dar es Salaam).

Ø  1981, mashairi yake ya Kiingereza yalishinda tuzo la BBC.

Ø  1979, alisaidiana na wenzake kuanzisha jarida la  Wimbi  lakini kutokana na sababu mbalimbali  hawakufanikiwa.
Maisha Ughaibuni
Alitoka Tanzania mwaka 1984 na bendi ya Sayari iliyochanganya muziki, dansi, ngoma, mashairi ya maonyesho na tamthiliya  wakazuru nchi za Scandinavia (Sweden, Norway, Denmark).  Baada ya miaka michache Ulaya alienda zake kusomea muziki, Brazil huku akipigia  bendi kadhaa hadi 1994 alipohamia Canada na hatimaye Uingereza.
Habari  zaidi na video zake tembelea : www.freddymacha.com

2 comments:

  1. Napenda kuwahamasisha wadau waende kwenye shughuli hizi. Freddy Macha nimefahamiana naye tangu miaka ya katikati ya sabini na kitu. Ninachofahamu zaidi ni vipaji vyake katika fani za uandishi na muziki. Ni mwandishi mahiri kwa ki-Swahili na ki-Ingereza, na ni kati wa-Tanzania ambao wamefanikiwa kuitangaza nchi duniani katika fani hizo. Ameishi na kutembelea nchi nyingi na kila anakopita ni balozi wa Tanzania. Uzoefu wake utawafaidia sana wadau.

    ReplyDelete
  2. Bahati mbaya ningekuwa karibu ningejitokeze ...Natumaini wengi watahudhuria

    ReplyDelete

Maoni yako