November 28, 2012

WARAKA KUTOKA MJINI LAHTI NCHINI FINALND


Na JACKLINE MLUGE-AUTIO, LAHTI-FINLAND

Wakati wote tunafikiria kuwa wenzetu wazungu wanapesa nyingi sana na ndio maana wanatusaidia. Lakini ukweli si kama wanapesa ila wana moyo wakufanya hivyo, ninasababu za kusema hivyo kwa sababu roho inaniuma kuona kuwa kuna baadhi ya watu ambao huwatesa watoto bila sababu ya msingi. Kila kukicha ukisoma katika magazeti mbalimbali ya Tanzania utakuta habari mbalimbali ambazo zinahusiana na kuteswa kwa watoto. Swali najiuliza kama kweli unamchukua mtoto wa mwezango kwa lengo la kumsaidia iweje leo umtese.
Kuna wangapi ambao wana moyo wa kuwatunza watoto wa wenzaao bila kuwatesa ni wakati umefika sasa Watanzania kuweza kubadilika ikiwa una mchukua mtoto wa mwenzako kwa lengo la kumtunza basi mtunze kweli na sivinginenvyo. Kuna usemi usemao kutoa ni moyo na si utajiri. Seija Saarikoksi Silvola ambaye ni  mama mwenye umri wa miaka 65 amebahatika kupata mtoto mmoja.
Jackline Mluge-Autio, akiwa na Mama Seija Saarikoksi nchini Finland.

Unaweza kujiuliza kwanini nimeamua kuandika makala hii? Nimeandika kwa nia ya kutoa changamoto kwa watanzania wenzangu kuweza kusaidia watu wengine hata kama tuna watoto zetu lakini pia kama unauwezo wa kusaidia inabidi tuweze kusaidia. Mara ya kwanza Seija, kufika bara la Afrika aliposhinda zawadi ya tiketi ya kwenda nchi ya kama unavyojua kwa mara ya kwanza kufika Afrika aliweza kuvutiwa na ukarimu wa watu ambao kwa nchi kama ya Finland ukarimu ni kitu kigumu sana.
Jackline Mluge-Autio akiwa na rafiki zake.
Mwaka 2007 alienda Tanzania na shirika la Settlement na baadhi ya wafini ambao walienda kutengeneza shule ya msingi Pekomisegese iliyopo mkoa wa Morogoro. Nakumbuka mwaka huo, mimi nilikuwapo ingawa sikuweza kukaa kwa muda mrefu kutokana na masomo. Tulikuwa tunalala kwenye mahema. Wafini walikuwa wanafanya kazi kwa kushirikiana na wakazi wa Pekomisegese. Na weza kutoa pongezi zangu na shukrani zangu kwa wakazi hao wa Pekomisegese kwani waliweza kushirikiana kwa hali na mali kwa kujitolea kuweza kujenga shule ambayo leo hii watoto wanaweza kukaa darasani na kujisomea.
Jackline akiwa na wanafunzi wenzake.
Mwaka 2009-2010 Seija na baadhi ya wafini walienda kujitolea kujenga shule ya msingi Pinda iliyopo Mgeta mkoa wa Morogoro. 2011-2012 shule ya msingi Tandale. Mbali na kujitolea kujenga shule pia Seija ana watoto zaidi ya kumi ambao anawasidia kwa hela yake mwenyewe bila kutegemea NGO. Ana wasidia kwa kuwalipia ada za shule na kuwanunulia vifaa vya shule. Sio kwamba eti Seija ni tajiri , la hasha ni ana moyo. Ikiwa mtu kutoka mbali anaweza kutusaidia je sisi wenyewe tunashindwa najua kabisa kuna mashirika ambayo yanasaidia watoto lakini pia mtu mmoja mmoja tunaweza kujitolea na kuwasaidia watoto wetu wa tanzania wenzetu bila kujali kabila au dini.  Kumsaidia mtu si mpaka umjue.

5 comments:

  1. kweli hii ni changamoto kubwa sana kwa sisi watanzania ..ambayo sidhani kama tutaweza...

    ReplyDelete
  2. Upo sahihi kabisa Yasinta inabidi tuwe na moyo wa kuwasaidia wenzetu wanao hitaji msaada

    ReplyDelete
  3. Hata wa-Marekani ni hivi hivi. Wanajibana ili watoe misaada kwa wengine, hadi kwetu Bongo. Kuna vijana hapa wameenda Bongo kujitolea, na wanapoona taabu za watu vijijini, wanahamasisha ndugu na marafiki kuchangia hela ili kuwanusuru waBongo. Utakuta wameanzisha maktaba vijijini, au wamepeleka vitabu, na pia kuwalipia ada watoto wasiojiweza.

    Lakini sisi wa-Bongo wenyewe michango yetu zaidi ni kwenye sherehe. Tukiombwa tupeleke hela za mchango wa arusi au "send-off" tunapeleka malaki ya shilingi. Gharama za arusi, ingawa ni mamilioni mengi, hazitutishi. Watu tunaunguza maelfu ya shilingi kila wiki kwenye ulabu.

    Lakini kuwachangia wenye dhiki, kwa mfano watoto yatima waweze kwenda shule, hatuwazii. Hata hao tunaowaita viongozi nao wana matatizo makubwa. Utawakuta wamewahi na mashangingi ya gharama kubwa kwenda kupokea madawati yaliyochangiwa na hao wazungu wa Ulaya au wa-Marekani, badala ya wao kuwa wachangiaji na wahamasishaji wa uchangiaji nchini.

    ReplyDelete
  4. Nadhani tatizo kubwa la watanzania hawana changamoto nakumbuka nilienda nchi moja walikuwa viongozi wa juu wa nchi hiyo wamekaa barabarani wakiomba hela ya kusaidia Afrika je kuna kiongozi yoyote Tanzania anaweza kukaa barabarani na kuomba hela kusaidia watoto wa afrika?

    ReplyDelete
  5. Good day! This is my first visit to your blog! We are a collection
    of volunteers and starting a neww project in a community in the same niche.

    Yourr blog provided us valuable information to work on. You have doje a extraordinary job!


    Feel free to visit my web blog ... company of heroes 2 cd key patch

    ReplyDelete

Maoni yako