March 21, 2013

TAMASHA LA PASAKA 'TUMAINI JIPYA KUNGURUMA MOROGORO


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph Mhonda, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa tamasha lao la ‘Tumaini Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Morogoro, linagusa hisia za wengi kwa kushirikisha wakali mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.

Mkurugenzi wa QS Mhonda, Joseph Mhonda(Katikati)
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mhonda alisema kuwa alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji  maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani Morogoro.

“Tamasha hili limeanzia Morogoeo lakini litaendelea kwenye m ikoa mingine ya Tanzania  likiwa na lengo la kutoa tumaini kwa jamii,  na mapato yatakayopatikana yatasaidia  watu walio katika mazingira magumu” alisema Mhonda

 Stara Thomas akiwa na waimbaji wa muziki wa injili 
Martha Mwaipaja
Alisema katika tamasha hilo ambalo ni la aina yake kufanyika Tanzania, litapambwa na waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki ambao ni Bahati Bukuku, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki, Stara Thomas, Matha Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven. Mbali na waimbaji hao  pia kutakuwa na kwaya mbalimali Rafiki Gospel Singers, Haleluya Kwaya, Victoria Kwaya na MTC .
Wahiriki wa tamasha la Tumaini Jipya Morogoro
Mhonda alisema sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia waimbaji hao pia watakuwa na muda maalum wa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa watu wote, pamoja na mbinu za kufaulu mtihani kwa wanafunzi.
Kwa mujibu wa waandaaji hao, Tamasha la Tumaini Jipya, ni fursa pekee kwa wakazi wa Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika kusherehekea siku Kuu ya Pasaka.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako