Ghasia zinazoendelea katika mji wa Tunduma ulioko mkoani Mbeya zimechochea uharibifu kijamii. Tunduma haiko katika hali nzuri. |
Vurugu kama hizo ziliwahi kutokea mjini Mwanza na kuhusisha wamumini wa imani ya kikristo na Kiislamu. Mauaji yalitokea na serikali ilifanya juhudi kuwakamata wahusika.
Hapa mwakilishi
wa Blogu ya Lundunyasa, anaelezea kwa ufupi sana juu ya kile kinachoendelea
mjini humo.
Ni kwamba inaelekea hotuba ya Rais
Jakaya Kikwete kuhusu uchinjaji bado haijaeleweka, hivyo wakristo bado walikuwa
na msuguano na wenzao juu ya nani achinje.
Tamko la Polisi lilisema
waislamu waendelee kuchinja sasa leo alfajiri vijana wa kikristo walienda
machinjoni na kumgawia kichapo cha kutosha mchinjajiwa kiislam ambaye
alifanikiwa kutoroka.
Baada ya hapo wakristo nasikia
ndiyo wakaanza hizo fujo ikiwemo pamoja na kufunga barabara, kuharibu msikiti,
kubomoa nyumba ya polisi mmoja aliyejenga uraiani, wameandamana na biblia mikononi
kudai haki ya kuchinja.
Polisi wa Tunduma kazi
imewaelemea na ikabidi nguvu itoke mkoani na RPC yupo huko sasa hivi. Juzi
kanisani Padre mmoja alitoa kauli kuwa kama hawa watu wanataka kuchinja basi
watuchinjie na kitimoto.
Kisa kikuu ni kwamba madalali wa
mifugo wamegoma kupima nyama zinazochinjwa na wakristo, hivyo wakristo wanahoji
kwanini iwe hivyo. Pia mtaani mabucha ya nyama zilizochinjwa na waislamu
zimeganda hakuna wanunuzi.
Raia ilibidi wakimbilie
mahakamani kwa kuona kwamba ndiyo sehemu pekee ya usalama kwao, hivyo ikalazimu
mahakama kuhairishwa ili kuepusha balaa. Kale kamchezo kakuchoma matairi na
kufunga barabara kakawa ndiyo mchezo wa kawaida.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako