May 01, 2013

CHEREKO CHEREKO ZA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO TANZANIA


Na Mwandishi Wetu,Cologne, Ujerumani

Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania Wanaoishi Ujerumani , chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) Waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana
kamili kwa maisha ya  mtanzania na binadamu wengine.

Sherehe hizo zilizowakusanya watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona  ya ujerumani, ziliutingisha mji wa koloni katika Usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya muungano wa Tanzania.

Mhe.Ali Siwa naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikua mstari wa mbele akiwaongoza watanzania katika Muungano Day,
Dada Nashe Mvungi akionyesha bidhaa za Tanzania kwa wageni

Dada Tabia Mwanjelwa(mwenye) gitaa akiwa na wasanii wenzie jukwaani

hakubaki mtu nyumbani

maana ya muungano yakubalika na watoto wa kimataifa !ngoma inogile

Mh.Ali Siwa,mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania,Berlin akitoa hotuba ya Ufunguzi,

Mh.Ali Siwa wa Ubalozi wa TZ Berlin,akizungumza na Mzee.Katabalo (mtumishi mstaafu wa UN)


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shah Smooth akiwarusha wageni
Muungano oyeeee! huyu dogo naye ndani ya nyumba
wageni mbali mbali wakiipongeza Tanzania, mwenyekiti wa UTU Mh. Mfundo aliyevaa shati la kitenge akiongoza shughuli
Mhe.Ali Siwa akiwa Msanii John Gambula kutoka Bagamoyo
Msanii Dada Joanita Henry(Mwenyeji wa muungano Day Koloni) akiwa na msanii mwenziwe kutoka Zimbabwe

Watanzania Ujerumani wakiduarika ktk Sherehe za muungani,mjini Koloni

wasanii wa kitanzania wakiepeperusha TZ katika maigizo n.k
wasanii wa kikundi cha Wabantu group wakiipeperusha TZ

wageni wakijichagulia Bidhaa za Tanzania


Wasanii mbali mbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi
kufanya mambo makubwa na kuitangaza  Tanzania kwa hali na mali chini  ya  Umoja wa watanzania Ujerumani(UTU)

No comments:

Post a Comment

Maoni yako