September 29, 2014

UTALII WILAYA YA NYASA




Na John Joseph, Liuli
 
Utalii ni sekta inayokua kwa kasi sana Duniani.Imechangia ktk kukua kwa uchumi wa nchi nyingi sana,imeongeza ajira nyngi sana,zipo zile za moja kwa moja na zingine ambazo si za moja kwa moja.

Sehemu zinazo wavutia sana watalii si mbuga za wanyama, si milima,si mapango bali fukwe nzuri na tulivu za bahari na maziwa.
Uswisi inajulikana kama 'the playing ground of europe' kutokana na ziwa dogo la Geneva,Visiwa caribean,Zanzibar,Mombasa na kadhalika zimekuwa zikiwavutia sana watalii kutokana kuwa na fukwe zinazovutia.
ufukwe uliopo mjini Liuli.
Ziwa Nyasa ni moja ya maziwa safi bado halijaharibiwa na shughuli za kibinadamu.Lina fukwe nzuri,safi na salama,maji meupe kwa ajili ya michezo mbalimbali...kama,mashindano ya kuogelea,mbio za madau au maboti.
Watu wa Nyasa,ili nionekane mkweli kuhusu fukwe zetu mi naonesha mfano-Ufukwe wa LIULI

No comments:

Post a Comment

Maoni yako