October 16, 2014

UVUVI WA KISASA WAANZA WILAYA YA NYASA
Sasa mambo yameiva wilaya mpya ya Nyasa. Kwakuwa maendeleo yameanza kuja kwa kasi kwa kuanzia sekta ya Uvuvi. Kama unavyoona pichani, hapo ni fukwe ya Mbamba bay kuna maboti ya kuvulia dagaa na samaki kwa wingi yakiwa na injini zake. Pia Teknolojia mpya ya matumizi ya umeme wa jua imeanza kutumika na wavuvi, hivyo kuokoa fedha nyingi kwa ununuzi wa mafuta ya taa kwa ajili ya karabai. Kwa kasi hii nadhani Halmashauri itapata mapato mengi, pia hata wananchi watanufaika. Hakika siku hizi samaki na dagaa ni wengi mno kwa kuwa Zana za kisasa zimeanza kutumika.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako