December 23, 2014

MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KWA WILAYA YA NYASA: CCM IMEJIROGA YENYEWENa Mwandishi Wetu, Mbamba Bay

1). KULETA PIKIPIKI ZA MKOPO KWA RIBA KUBWA: Pikipiki zimekopeshwa kwa sh. 2,380,000/=, malipo kwa mwezi ni zaidi ya sh.1**,000/=. Kwa miezi 18. Sasa wenye MIRADI INAKUFA na wengine wanawaza KUTOROKA MIJI.

2). KUTOTUMIA BUSARA KUWASIMAMISHA WAGOMBEA WASIOFAA NA WALIOSHINDWA KAZI KAMA KIJIJI CHA MBAMBA BAY. Mbamba bay ni makao makuu ya wilaya lakini chama hakikutumia mawazo kumsimika Mgombea Mwenyekiti kijiji ambaye hakuna alichokifanya na hawajali wananchi wake. Mwishowe yake wamefeli.

3). KUTOWAJALI WANANCHI WA WILAYA YA NYASA KWA SERA MBOVU ZISIZOTEKELEZEKA.

4). KUDANGANYA UMEME UNGEWAKA MWEZI NOVEMBA 2014. Hadi sasa ni nguzo tu zimesimikwa. Hakuna Nyaya, pia kituo cha TANESCO kuota nyasi tu.

5). KULA HELA ZAIDI YA SH. MILIONI 400 za WANANYASA kwa kivuli cha NYASA FOUNDATION Feki isiyo na ofisi na wajumbe wake hawajulikaniki.

6). KUUZA CHEM-CHEM ZA MAJI KWA WATU BINAFSI, huku wananchi wakiteseka bila maji na kuumwa matumbo kwa maji ya mgao. Wakati wengne wanakesha nayo 24 hrs.
7). KUWANYONYA WANANCHI KWA MICHANGO ISIYO NA TIJA KWA WAkazi wa Nyasa.

Itaendelea ..............!!! 

No comments:

Post a Comment

Maoni yako