September 15, 2017

KENYATTA: MARUFUKU KUSAFIRI NJE

NAIROBI, KENYA
Serikali ya Kenya imepiga marufuku kusafiri nje ya nchi bila idhini maafisa wake. Kupitia taarifa rasmi kwa maafisa wa serikali ambayo TUKO.co.ke imesoma, Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua alisema Mawaziri, Makatibu wa Wizara, Maafisa katika Wizara, Wakuu wa Mashirika na maafisa wao hawaruhusiwi kusafiri nje ya nchio bila ya idhini kutoka kwa Rais. 

Nakala za barua hiyo zimetumwa katika wizara muhimu zinazohusika na uhamiaji ikiwa ni Wizara ya Ndani na Ushirikishi wa Serikali ya Kitaifa na Wizara ya Mambo ya Nje. ''Hii ni kufahamisha kuwa, imekubaliwa kwa,mba, hadi kuamliwa vinginevyo, hamna Afisa wa Serikali atasafiri nje ya nchi bila ya kibali kutoka kwa Rais. Ili kuondoa, maafisa hao ni pamoja na Mawaziri, Makatibu wa Wizara na Maafisa kutoka Wizara, Maafisa Wakuu wa Mashirika na Maafisa wao, na Wakurugenzi wa Mashirika ya Serikali." Barua hiyo ya Jumatano, Septemba 13 2017, ilisema.



No comments:

Post a Comment

Maoni yako