November 01, 2017

FURSA: MAFUNZO YA JESHI JKT 2017

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo anawatangazia vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2017.
 
Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa mikoa na wilaya ambapo muombaji anaishi.

Zoezi la kuchagua vijana litaanza Mwezi Novemba 2017 na vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 04 mpaka 09 Desemba 2017.



Jeshi la Kujenga Taifa linaendelea kusisitiza kuwa nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya JKT haziuzwi, aidha yeyote atakaye husika na utapeli wa kuuza au kununua nafasi hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Sifa za mwombaji ni kama ifuatavyo:
1. Awe raia wa Tanzania.
2. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la Saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.
3. Vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne ni kuanzia miaka 18 hadi 20.
4. Vijana wenye elimu ya Kidato cha Sita ni kuanzia miaka 20 hadi 22.
5. Vijana wenye elimu ya Stashahada na Shahada ni kuanzia miaka 23 hadi 25.
6. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamili ni kuanzia miaka 26 hadi 27.
7. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu ni kuanzia miaka 28 hadi 35.
8. Awe na afya njema, akili timamu na asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo).
9. Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
10. Kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari kidato cha nne, wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2015, 2016 na 2017 wenye ufaulu wa alama (Points) zisizopungua 32.
11. Awe na cheti cha elimu ya msingi aliyehitimu Darasa la Saba.
12. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
13. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving Certificate).
14. Awe na cheti halisi cha matokeo (Original Academic Certificate) na kwa wale waliomaliza shule mwaka 2017 wawe na Transcript au Statement of Result.
15. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.
16. Asiwe amepitia mafunzo ya JKT Operesheni za nyuma.
17. Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo.
18. Aidha, Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa na pia kuwa na vifaa vifuatavyo:
19. Bukta ya rangi ya Dark blue yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu. Aidha bukta za wanawake zinatakiwa kuwa na lastic magotini.
20. Raba za michezo zenye rangi ya kijani.
21. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
22. Soksi ndefu za rangi nyeusi.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 30 Oct 2017

No comments:

Post a Comment

Maoni yako