NA
HONORIUS MPANGALA
Kwanza
mtoto wenu nimefika salama kutoka safari yangu ya Dodoma. Nishafika kwa Mbaraka
Mwishee salama. Leo naomba nishiriki nanyi haya yawezekana yalikuwa
yananisumbua kila siku halafu nilawa naogopa kuwaambia wenzangu ukweli. Lakini
kuna mtu anaitwa James Chiggs ni kama amenifanya nami niondoe ile hofu ya
kufikiriwa tofauti. Kama naweza kutukanwa na mashabiki Wa Simba na Yanga
kutokana na Kalamu yangu kwanini niogope kwa nyie ndugu zangu.
Miaka
ya Nyuma aliwahi kutokea mmoja Wa viongozi Wa kisiasa kwa ngazi ya uwaziri
aliitwa ALFRED TANDAU nafikiri mnamfahamu nyie Wanyasa na hata Watanzania kwa
ujumla kwani alikuwa Waziri Wa mawasiliano.
Hadi
naondoka Duniani hakuna unachoweza kusema hii ni alama ya Tandau aliyoifanya
Nyasa.
Miaka ikaenda tukapata mwakikishi Wa wananchi kupitia jimbo la Mbinga
Magharibi Mh. Tadei Luoga kila mmoja anakumbukumbu za huyu mtu sitaki kusema
kwasababu sio vyema kuwazungumzia watu ambao mwenyezi mungu aliwachukua kwa
ubaya walioufanya. Hata Jambazi kwao wanafanya matanga.
Kuna
kosa kubwa ambalo limekuwa la muda mrefu kutokana na yale yaliyotokea kwa
mababu zetu. Imani potofu ilikimbiza watu yawezekana hata malalamiko
yanayotokea sasa ni mshahara Wa mbegu chafu iliyosababishwa na mababu waliokuwa
magwiji na wakawafanya vijana Wa zamani wakakimbia kwetu kwasababu za
kujisalimisha.
Leo
hii mandeleo ya Nyasa tunapoyahitaji kwa jicho la kuyapigania lakini tunapaswa
kufahamu wako ambao mioyo yao ilishakufa kutokana na mambo waliyofanyiwa na
mababu miaka hiyo. Hivyo uwepo wao katika kitengo fukani bado kunawapa shaka ya
kuwa wenye kuhitaji harakati za kweli juu ya maendeleo ya Kwetu.Siwezi kuwalaumu
sana kwa waliokutana na changamoto ya namna hiyo.
Lakini
pia baada ya Luoga alifuata Kepten Komba. Sitaki kumzungumzia kwa ubaya wake
wala uzuri wake kwasababu ameshatangulia mbele ya haki.
Maendeleo
ya mahali huletwa na watu na sio ngedere au Mbuzi. Hakuna kitu kinakikera kama
hizi harakati ambazo wanazifanya wanyasa walioko mjini kwa kuonekana wanajua
mambo kwa kutolea mifano mbalimbali lakini hawajawahi kufika eneo husika ambalo
wao hujisemea ndo kwao.
Utasikia
kikao cha wanyasa waishio Dar es salaam kitafanyika Lamada. Kudadadeki
mnashindwa kwenda Nyasa mnajifanya mnakusanyikia mjini. Kama unaona Nyasa sio
kitu kwako kwanini uusemee moyo kwa kutaka kuonekana machoni pa watu ni
miongoni mwa wapigania maendeleo ya Nyasa halafu una miaka 10 mjini hata Nyasa
huijui. Halafu mnasema oneni wezetu wachaga sijui wanafanya moja mbili tatu. Mi
najiuliza uliwahi kwenda Nyasa ukasikia wanachokisema usiishie kupiga simu.
Wilaya
ya Nyasa kama inavyotambulika ina tarafa tatu. Yaani Mpepo Ruhekei na Ruhuhu.
Hakuna tafara imekosa watu Wa kuisemea kama ya Ruhuhu. Hakuna uwiano wa miradi
kati ya tarafa hiyo na hizo zingine. Wakati barabara ya Kitai hadi Lituhi iko
chini ya Tanroad lakini hakuna anayekumbuka hata kuuliza labda kwa wahusika
hivi na kule vipi.
Yawezekana
Mimi niko karibu sana watu wa tarafa ya Ruhekei kutokana na kupata kwangu elimu
ya Sekondari Liuli na pia Mamangu Binti Machusa kwao Ng'ombo hivyo Ruhekei kwa
wajomba na Ruhuhu kwa Baba. Huwa naumia rohoni ninapoona harakati za kuifanya
Nyasa ifanane na Msoga au Chato inafanywa na Wanyasa Wa Ruhekei pekee najiuliza
hivi wale Wa Ruhuhu ni kweli wamesusa kwao.
Hakika
kama kutelekezwa basi rumetelekezwa kwelikweli. Maana kila niki fikiria adha
tuipatayo kwa upande Wa Mawasiliano na uchukuzi najiuliza hivi kama serikaki inasema
inapeleka maendeleo kwa wananchi ,hivi hao wananchi ni Wa maeneo gani?.
Wakati
komredi Komba alipokuwa madarakani aliboost kidogo watu Wa kata ya Lituhi
wakapata Unafuu Wa mawasiliano ya simu. Ilijengwa minara kama mitatu haraka.
Miaka
ya karibuni nimeshangaa kampuni ya Tigo kwenda kujenga minara mitatu katika
eneo ambalo liko ndani ya km 10 wakati kijiografia ya Nyasa hata minara miwili
ingefaa na kuongeza km zingine 10 na kupata km 20 zenye minara mitatu kutokana
na jiografia ya Nyasa kuwa ya milima hivyo kusingekuwa na shida yoyote katika
nguvu za mvutano kutoka mnara moja hadi mwingine.
Mwaka
wa tatu mnara wa Halotel uliojengwa mlima "Lilengalenga" kijiji cha
Lundu haufunguliwi na kuwasaidia wakazi wa maeneo ya jirani kuwasiliana. Sasa
walijenga wa nini si wangeacha tu.. Kila siku sarakasi ambazo hazina majibu
stahiki kwa wahusika.
Hakuna
watu wana shida ya mawasiliano kama kata ya Mbaha, Ngumbo na Liwundi. Sio kama
tumeridhika ila iko siku mkija na shangingi zenu mtapigwa mawe sana kwasababu
ya utapeli ambao wanasiasa mnaufanya. Na haya maeneo yana madiwani walewale
ambao sifa yao Kuu ni KKK. Sasa unafikiri watamwanbia nini mkurugenzi.
Mwaka
juzi niliwahi kusema mimi sifurahii mbunge wa jumbo letu kuwa waziri na hata
kesho ukiniuliza kwanini nitakupa sababu ninazo amini. Wengi mlimpa sana
pongezi Stella Manyanya lakini hamkujua kazi kubwa anayotakiwa kuifanya ni ipi.
Ndo
maana hadi leo bi mkubwa tangu achaguliwe hajawahi pita vijiji vyote na kuongea
na wanachi wake. Matokeo yake mnatimuliwa vumbi tu huku ndugu zangu wakipunga
mikono. Hapo ujue anaenda kwenye Tamasha la Utalii.
Naunga
juhudi za utalii kwa Nyasa lakini kuna mahali ubongo wa wengi akiwemo Manyanya
ume- stack kama kompyuta. Utawezaje kutangaza vivutio vya utalii wakati huko
unakokutangaza hakuna barabara ya uhakika ili watalii wakafika na kuongeza pato
kwa kuwekeza?
Barabara
mbovu sasa huyo mtalii atakujaje. Atatumia usafiri gani ili afike. Kucheza
ngoma na kula nyama sio mwisho Wa kuutangaza utalii tunaoutaka lazima tuumie na
kuumia kwenyewe ni kuhakikisha miundombinu iko Sawa.
Wakati
watanzania wakiwashangaa wasukuna wa Bariadi kwa kumchagua Chenge itabidi
muwaulize ni kipi anachowafanyia wale hadi waendelee kumuweka madarakani.
Achana
na harakati za kuikomboa Nyasa ila kiukweli mko wengi mlioko mjini na mmesusa
kwenda kusaidia hata kwa mawazo juu ya nini kifanyike kwa wanyasa wenzenu.
Kwa
macho yangu nimeshuhudia watu wanafikia alikoolewa Dada yao na kwao hakuna mji
kwasababu tangu wazazi wafariki basi watu wamekacha hata kwenda kwao.
Sasa
ukienda ndo unafikia kwa shemeji yako. Wako wanaofikiri ni ujanja kupotela kwa
watu na kukaa miaka mingi mikoa ya watu bila kwenda Nyumbani.
Nilisafiri
na Mzee mmoja ambaye aliniambia aliondoka Mbinga akiwa na miaka 30 na kakaa
Tanga miaka 30. Tukiwa kwenye gari sikutaka kumvumilia nikamwambia huo sio
ujanja Mzee ni ushamba kwasababu unajionyesha wewe ni mtumwa wa fikra. Huwezi
jisifia kwa waelewa kuwa sijaenda nyumbani miaka 30.
Sasa
wako waliokuwa kama huyu Mzee na wanajitambulisha ni Wanyasa na hujifanya
wanatoa maelezo mengi kuhusu Nyasa ya zama zao. Kutokana na kawaida yetu ya
kuwaona walioko mjini ni miungu watu ndo maana wanyasa wakichinjiwa Mnyama tu
tayari wanakuona kama mfalme wao.
Elimu
ya kujitambua ndugu zako huwezi itolea kwa mikusanyiko ya Lamada au msimbazi
bali nenda kwa wanyasa kulekule kaongee nao..
Binafsi
nimepanga kama mbungu atanipa uhai kuanza na darasa la kujitambua kwa wanyasa
pamona na elimu ya uraia kwa kata ya Mbaha. Ndani yake nitakuwa na elimu ya
kufuata fursa kwa kujiinua wenyewe katika familia zao.
Yawezekana
hakuna niliyewahi kumwambia lakini najua nafasi ya kuongea na Ndugu zangu Wa
Mbaha nitapa haya mambo yakuuza utu kwa vimboma vya nyama vinatuonyeaha jinsi
gani hatuna elimu ya utambuzi katika masuala ya msingi kwenye maendeleo.
Mungu
endelea kunipa uhai ili yale ninsyoyafikiria kwa jamii yangu yaweze kutimia.
Nimechoshwa na wanasiasa kwabkiasi kikubwa sana kwasababu wanawadanganya sana
bibi zangu babu zangu kaka zangu na wengine.
Kama
kuna mtu nitakuwa nimemkwaza we umia tuu kwasababu sina mpango Wa kumwomba mtu
msamaha kwa haya.
Acheni
ulimbukeni hizo kanda zilizoendelea hazikufikia hivyo bila watu kupeleka
maendeleo kwao. Halafu ubataka Nyasa ifanane na uchagani wakati we kwenu huendi
unasema kuna wachawi huu ni ushamba. Tunaoenda hawatuoni?
Keneth Kondowe Lihambanda's sauti
unayopaza sasa inafaida kesho. Chiggs endelea hivyo hivyo yawezekana ndoto ya
kuwa Robin Hood ikatimia kwako.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako