March 02, 2018

MO IBRAHIM,INUKA JIPUKUTE VUMBI UENDE

Na.Honorius Mpangala
MABADILIKO ya bechi la ufundi katika klabu yoyote huja na matokeo chanya na hasi kulingana na mwenendo wa timu au klabu kwa ujumla.Katika hilo kuna mambo huenda yakawa tofauti kwa wachezaji walioonekana kupata sana nafasi kabla ya mabadiliko.Unayakumbuka maisha ya mchezaji wa Chelsea John Mikel Obi baaada ya kutumuliwa kwa Jose Mourinho pale klabuni.Ujio wa Guus Hindik ulirudisha kwenye hali ya kupata nafasi hadi kufikia hatua ya mashabiki wa kitazania walimpachika jina la Ombeni Sefue.

Kupachikwa kwa jina la Ombeni Sefue kwa Obi kulitokana na jinsi alivyoonekana kutotumika wakati wa Mourinhona alipofika Hidink akaanza kumpa nafasi.Hii ilifananishwa na Sefue wakati wa utawala wa awamu ya tano alivyokuwa hasikiki katika serikali hadi ilipoingia serikali ya awamu ya tano.


Mabadiliko ya makocha yanakuwa yenye kuleta mabadiliko katika vikosi kutokana na kila kocha hupenda kuja na falsafa zao.Hili ndilp lililomkumba mchezaji fundi wa mpira aliyepita katika mashamba ya miwa pale Manungu Turiani Mohammed Ibrahim.Hadi klabu ya Simba inafikia hatua ya kukubali uwezo wake na kumsajili ni kutokana na kile alichokuwa akikifanya akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar.

Simba waliamua kufanya usajil ulijumuisha wachezaji watatu kwa pamoja toka Mtibwa sugar yaani waliwasajili Mzamiru Yassin,Shiza Kichuya nay eye Mo Ibrahim ambao walikuwa mhimili mkubwa wa klabu hiyo yeneye maskani yake katika mashamba ya miwa Manungu Turiani.

Wajihi wa Mo Ibrahim ilikuwa mija ya kumfanya natofuatiane na wenzake kimwinekano kwani alikuwa kafuga rasta hivyo kwa uwezo wake ilikuwa ni kitu chepesi kutambua uwezo wake kwani alionekana sana.Lkini hali imekia tofauti sana mara tu alipotua katika klabu ya Simba.Hatumwoni tena uwanjani mara kwa mara,sio kama uwezo wake umepungua hapana ila ni matumizi ya mbinu za kisoka ambazo kocha anaweza kuona kuwa watu Fulani wananifaaa katika mbinu hii na hawa hawanifai katika mbinu hii.

Wakati wa usajili wa dirisha dogo msimu huu ziliibuka tetesi za yeye kutaka kuondoka katika klabu hiyo ili akapate muda wa kucheza katika klabu nyingine na alinde kiwango chake.Hii ilitokana na tangu ujio wa Joseph Omog kulifanya Mo awe na muda mchache sana wa kuonekana uwanjani akicheza tofauti na ilivyo kuwa kwa Jackson Mayanja wakati huo anainoa simba kama kocha mkuu.

Omog alifanya Mo awe anayepata muda mcheche na baadae kutomtumia kabisa pale alipokuja kocha msaidizi mwingine Masoud Djuma Irambonaimana.Madiliko ya klbu ya simba ya kumtimua kazi Omog na kucha mikoba kwa Irambonaimana kukafanya Mo apotee kabisa katika kikosi. Hii ni kutokana na machagulio ya kocha katika kufanikisha mbinu zake za kimpira.Kupotea kwake kumefanya aibuke Nickolas Gyan ambaye alionekana kutopata nafasi mbele ya mtamgulizi wa Irambonaimana.

Licha ya kwamba hali hiyo imeweza kumkuta hata mchezaji Mohammed Hussein lakini yeye ni kutokana na kuletewa msaidizi wake ambaye kaja na akafanya vyema sana. Kumbuka Zimbwe jr ndiye aliyekuwa amecheza mechi zote za simba msimu uliopita akifuatiwa na mkongomani Javier Besela Bukungu.Sasa benchi laufundi lilikuwa na haja ya kumlrata msaidizi wake ndipo walipomsajili Erasto Nyoni n baadae wakamleta pia Asante Kwasi.

Utofauti wa Mo na Mohammed Hussein unatokana na kile kinachoonekana kuwa kiungo huyo hana nafasi ya kucheza wakati hata kuipata hiyo nafasi ya kuwaaminisha mashabikia na wakarizika na kinachofanywa na benchi la ufundi wakione kiko sahihi.

Kwa idadi yao kama walivyoka Mtibwa sugar nyota ilikuwa imeng’ara kwa Shiza Kichuya na Mzamiru licha ya kwamba nae kwa sasa amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza dakika zote kama ilivyo kuwa awali kutokana na uwepo wa kiraka James Kotei na Nyoni ambao wanlifanya nechi na ufundi kuina lina uwanja mpana wa kuchagua kikosi kulingana na uwezozwa wachezaji ambaounakuta wanacheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.

Ujio wa kocha Pierre Liechantre kumefanya Mo azidi kupotea machoni kwa wapenzi wa klabu ya simba kutokana na kuwepo kwa mwendelezo wa kutopata nafasi ya kucheza.Iliwahi kumkuta mchezaji Paul Nonga ambaye alitoka Mwadui na kujiunga na klabu ya Yanga na akawa na ufinyu wa kuapata nafasi ya kucheza.Alisajiliwa dirisha dogo kwa mkataba wa miaka miwili lakini aliitumikia Yanga kwa miezi sita na akawepo katika kikosi kilichoipa yanga ubinwa na baadae akaomba kuondoka na uongozi ukaridhia kwa matakwa yake aliyoeleza.Unaweza kusema alioogopa kupigania namba lakini kiuhalisia alienda Yanga huku wakiwa na wachezaji wanaocheza eneo la ushambuliaji kama Donald Dombo Ngoma,Amis Jocelyn Tambwe,Obrey Cholla Chirwa ilikuwa ngumu kwake kupenya kwa washambuliaji hao na akaanza badala yao.Maamuzi aliyoyafanya ilikuwa kwenda katika klabu ambayo atapata muda wak kucheza kuliko Yanga.

Mo ukiinuka hapo katika benchi au huko jukwaani na kujipukuta vumbi na kwenda zako mahala pengine hutoonekana mjinga bali utakuwa umetoa maamuzi ya kiume na yenye kila chembe chembe ya mafanikio. Ni ngumu sana kufanya maamuzi kuziacha hiziz timu za kariakoo lakini yawezekana matunda ambayo utayapata baada ya nkwenda utakako ona watatunza kipaji chako basi utafurahia. Nyakati zote ni ngumu kufanya maamuzi kuondoka unapopapenda lakini uhalisia wa kama ulikuwa sahihi kutoka au kuto kutoka utakuja kuona ukiwa nje ya hapo.

Kwa uwezo wa Mo sio mchezaji wakukosa nafasi uwanjani kwani anaweza kama kutumika kama kiungo wa pembeni akiwa na jukumu la kusaidia kiungo cha kati,pia anamudu kucheza nyuma ya mshambuliaji na hata kiungo mchezeshaji.Kama unakumbuka katika klabu ya Mtibwa kiungo cha chini na juu walisimama Shaaban Nditi na Mzamiru Yassin na kulia na kushoto ndiko walikocheza Mo na Kichuya.

Katiika klabu ya simba alikuwa akitumika hivyo hapo awali lakini ujio wa Haruna Niyonzima ukafanya lile eneo ambalo yeye alilicheza kwa ufasaha linachezwa pia na mnyarwanda huyo.Hali hiyo ikafanya Mo kuwa na hatiahti ya kucheza kila mchezo,majeruhi ya Niyonzima hayaweza kumpa tena nafsi kwani tayari kwani Saidi Ndemla kashika kasi hivyo kutokana na uwepo wa viungo wengi na simba wanakawaida ya kupenda soka lakuoiga psi nyingi inawafanya wawe na winga mmoja tu asilia na winga nyingine kuchezwa na mtu wa kiungo kama ilivyo kwa Ndemla anavyofanya.

Wako wachezaji wengi walioonekana kutokuwa na lolote katika klabu ya Simba lakini walipoenda kwingine wakarejesha ukali wao.Ilitokea kwa nahodha wa Mtibwa Shaaban Nditi alisajiliwa simba lakini mambo hayakumyokea akarejea Manungu hadi leo anaendelea na soka lake.Pia mmoja wa wafungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Abdallah Juma alitokaMtibwa kwenda Simba hakuweza kufanya lolote ndani ya wanamsimbazi akaamua kurejea tena shambani manungu na akarejesha ukali wake uleule.Hivyo kuna kila sababu ya kujitazama tena upya kwa Mo Ibrahim ili alinde kipaji chake.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako