February 28, 2018

SIKU YA MASHUJAA SONGEA


Wanafunzi wa shule mbalimbali wa Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wakiliangalia kaburi la Nduna Songea Mbano, aliyezikwa kiwiliwili tu na kichwa chake kupelekwa Ujerumani, kwa kuwasumbua wajerumani kukata kamba ya katani Mara tatu na baadaye kupigwa risasi. Mashujaa wengine 65 walizikwa katika kaburi moja halaiki. Leo ni kumbukizi za mashujaa wa vita vya majimaji walionyongwa miaka 112 iliyopita. (27.02.1906).

PICHA NA JUMA NYUMAYO

NAFASI ZA KAZI MAMLAKA YA BARABARA VIJIJINI "TARURA" MKOA WA RUVUMA

 
 

SERIKALI IMESIKIA KILIO CHA WENGI

NA GABRIEL MWANG’ONDA
HATIMAYE serikali imesikia kilio chetu kuhusu Single Customs Territory (SCT), wakati mfumo huu ukianzishwa na kutumika hapa kwetu Tanzania, binafsi nilipinga sana japo yalikuwa ni maazimio ya jumuiya za uchumi za Afrika Mashariki na SDC countries walikuwa ndio wanaanza kuipigia chapuo.
Mfumo huu unahusisha maafisa wa Forodha kutoka nchi jirani kuja kuweka kambi katika bandari yetu ili mtu akisema anaingiza bidhaa na zinaelekea DRC kisha aende kwenye deski la DRC lililopo hapahapa bandarini kwetu na kulipa kodi zote pale Bandari ya Dar es salaam. Kifupi ni kwamba sisi tulikuwa tunasaidia nchi jirani kudhibiti ukusanyaji kodi.
Mfumo huu ulilenga pamoja na mambo mengine kudhubiti wizi mkubwa wa bidhaa zinazokuwa zinanasinishwa kwamba ziko in transit wakati si kweli kwamba ni transit, mara nyingi huishia mikoa ya karibu na Dar es salaam na kurudi sokoni hapa nchini. 

February 26, 2018

RIWAYA: SAA 72

Ijumaa iliyopita ndugu Japhet Nyang’oro Sudi aliwasiliana nami kunijulisha kuwa nimetunukiwa zawadi ya kitabu chake. Yeye ni mwandishi wa riwaya ya SAA 72. Hima jumamosi nikawasili kwa bwana George (Muuza vitabu huyu; simu yake; 0713 454152). George huuza vitabu vyake pembeni ya sanamu la Askari  jijini Dar es salaam (Posta Mpya). ana vitabu vingi, waweza kulonga naye kujipatia nakala zaidi. Nilianza kusoma kitabu hicho Jumapili asubuhi yapata saa 4 hivi, hadi saa 2 usiku. Nikatamatisha. Kina kurasa 202.
Masimulizi ya kitabu hiki ni kuhusiana na mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Joseph Katanga anaachiliwa huru na Makahama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa madai ya kubadilika kitabia). Lakini Katanga hakubadilika chochote. Alitumia kila njia kuendesha maasi kwa wanavijiji, na kudhoofisha utawala waDRC. Machache tunayoweza kujifunza.

ZAWADI YA VITABU KWA MARA NYINGINE

JUMAMOSI Februari 24 mwaka huu nilipatiwa zawadi ya vita viwili kutoka kwa Bwana Ragin Mmbaga, kama vinavyoonekana pichani. Vitabu hivyo vimeandikwa na Bwana Johne Wisse. Kuna kitabu cha TONE LA DAMU cha lugha ya kiswahili na THE BROKEN CAMPUS RULE cha lugha ya Kiingereza. 
Ninawashukuru kwa kujali kuwa visima vya maarifa. Hakika mwaka huu nimeanza kwa furaha kubwa kwani huyu anakuwa mtu wa tatu kuniletea vitabu kibaruani kwangu. 

Usomaji wa vitabu ndicho kitu ninachokipenda zaidi. Ndicho kilevi au kitu ambacho kinachukua muda wangu wote kuhakikisha nafurahi. Zaidi ya hapo navutiwa na mchezo wa soka. Vitabu ni kitu muhimu sana. Namshukuru Ragin Mmbaga kwa niaba ya John Wisse. ASANTENI SANA

-MARKUS MPANGALA

WAMACHINGA WA KIZUNGU NDANI YA MJI WA MOROGORO

Nimewanasa mwenyeeeeewee kwa kamera yangu. Msamvu Morogoro,wanauzia bidhaa abiria Wa kwenye magari. Jana nilimnasa mmoja katika mgahawa uliopo maeneo Stand ya daladala ya mjini kati moro nami nikawa mmoja wa wateja wake. Wakati sisi tukiwashangaa wenzetu wanapiga hela wanaondoka. Vyuma vimepata grisi ya kizungu.
 PICHA; Honorius Mpangala

February 23, 2018

KAMBALE SAMAKI WA AJABU KULIKO SAMAKI WOTE DUNIANI

NA JACOB MALIHOJA
 
NIMEFUATILIA kwa kina samaki wa aina tofauti wa ajabu kama vile Electrical El (Mwenye uwezo wa kuzalisha umeme hadi Volts 900 yaani mara nne ya umeme tunaoutumia majumbani), 

Ngisi mwenye uwezo wa kujibadili rangi kama kinyonga kulingana na mazingira anayokuwepo na mwenye nguvu kubwa za kung'ata kuliko nguvu za kung'ta za simba, au Nyangumi kwa ukubwa wake .. binafsi nampa namba moja Kambale baada ya kugundua ni samaki pengine yaweza kuwa kiumbe wa kwanza kuishi mahali kwa miezi au miaka bila kupata chakula.

MBOGA 7


Ukiwa mji kama wa Dar es salaam utasikia stori nyingi za Mboga 7. Au ukiwa maeneo ya mijini hii stori ya mboga 7 imezoeleka sana kusimuliwa. Lengo ni kuelezea familia yenye uwezo wa kuandaa mlo mmoja ukiwa umesheheni mboga za kila aina(nyingi). Lakini kwa wakazi wa Nyasa na Kijiji cha Lundu suala la Mboga 7 ni kawaida sana. Tofauti iliyopo ni kuelezea mazingira tu. Pengine watu wa mjini “Mnalamba lamba tu, hamshibi kisa hamna mboga”. Njoeni Lundu.

HEKIMA ZA BIBI KIJIJINI


NA JOHN  CHITANYA
 
MJUKUU wangu Irene;
WACHAFU wengi wanatabia ya kuvaa nguo safi.
"Ngono haiwezi kumfanya mwanaume asimuache mwanamke, Hata kama huyo mwanamke awe fundi vipi!
UZURI wa mwanamke unaweza ukapelekea mwanaume akathubutu kumuoa, Lakini TABIA yake ndiyo itakayo mwamulu atadumu Kwa muda gani na huyo mwanamke katika NDOA hiyo.
Mjukuu wangu Irene; UZURI pasipo kuwa na TABIA NJEMA hauwezi ukapata mume bora. Sana sana unaweza ukapata Boyfriend tu, na ukawa unatembea na Wanaume za watu. Kuna Mambo mengine Pesa haiwezi kununua, vitu km HESHIMA, BUSARA na UPENDO.

Mjukuu wangu Irene; Kuwa mtamu katika Tendo la Ngono, Inaweza Ikamfanya Mwanaume alale na wewe Usiku kucha, Lakini Asbuhi akaondoka Zake. LAKINI KUWA MTAMU KATIKA TENDO LA TABIA, Kunaweza kukamfanya mwanaume AKUOE na ADUMU na wewe mpaka Kufa"
Wasalaam
Thekla Frank Machusa.
Bibi yako.
*Mbio zetu Kabla ya Uhuru*

RAIS ATOA VIFAA TIBA MANISPAA YA SONGEA

NA MWANDISHI WETU, SONGEA
 
RAIS wa Tanzania Dk.John Magufuli ametoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya milioni 18 kwa ajili ya zahanati za Halmashauri ya Manispaa ya Songea lengo likiwa ni kuboresha huduma ya afya kwa wananchi.
Vifaa vilivyotolewa ni vitanda 20 vyenye thamani ya shilingi 7,920,000,mashuka 50 yenye thamani ya shilingi 510,000,vitanda vya kujifungulia vyenye thamani ya 6,108,800 na magodoro 20 yenye thamani ya shilingi 3,670,000.
 Mbunge wa Songea mjini Dk.Damas Ndumbaro ndiye aliyekabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika hafla fupi iliyofanyika katika Kituo cha Afya Mjimwema.

Mbunge wa Songea Mjini Dk.Ndumbaro amesema kukabidhiwa kwa vifaa tiba hivyo ni moja ya ahadi ambazo aliahidi Rais wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu
Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea Dk.Mameritha Basike amesema vifaa hivyo vitagawiwa katika baadhi ya zahanati zilizopo katika Manispaa hiyo ambazo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa hivyo.

SEKTA BINAFSI KWA MAENDELEO YA UCHUMI WA AFRIKA YA MASHARIKI

AJENDA: Afrika ya Mashariki.
WENYEJI; Uganda
WAHUSIKA: Ndugu Rais Yoweri Museveni, ndugu Rais John Magufuli na ndugu Rais Uhuru Kenyatta
MADA: Sekta binafsi kwa maendeleo ya nchi za Afrika mashariki.
MAONI: Sekta binafsi ina lengo la kutafuta faida. Haitatokea kuwa utoaji wao wa huduma kuwa kigezo cha kutotafuta faida. Ni jukumu la serikali kusimamia kupata haki zake kutoka kwa wadau wa sekta binafsi kwa njia zinazofaa. Tukitaka kuilazimisha sekta binafsi isilenge faida tutarudi kwenye "Mashirika/viwanda vilivyobinafsishwa" enzi hizo na baadhi yao kuwa "ghala za popo".

--MARKUS MPANGALA

AFYA: WATANI ZETU WANA NACHINGWEA, SHIRIKINI KATIKA ZOEZI LA MATIBABU YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA