March 31, 2008

Ndogondogo na Masuala Muhimu ya Wanyasa

Sikujua niandike nini leo hii kwani nilijikuta hii kompyuta inikikasirisha sana,nikataka kuipiga ngumi,lakini nikapiga ngumi hiyo kifuani na kichwani.Sikuishia hapo nikatwanga ngumi nzito ukutani labda itanielewa kwamba sipendi inavyonisumbua eti hakuna mawasiliano.Nikaona sasa naaibika kweupe hivi.Lakini nilijikuta nikiumia mwenyewe na ghadhabu zikaishia na kompyuta ikakubalia ndiyo maana nikaandika ndogondogo za wanyasa.Wanyasa wanaanza kusahau kuhusu nyakati maalumu kwani bila shaka aprili hii inavyoaanza basi mambo ni yaleyale ya kuvua sana samaki na kulima kwa kasi ili kujipataia chakula cha asili.Sasa ni mwendfo wa kulima na kuvua,ngoma zimesahaul;ika ingawa watu bado wanachembechembe za kuselebuka na kunywa pombe zao,lakini dadangu kanikumbusha kuhusu Myakaya mm,ndiyo maana nasema wanyasa ni wanyasa jamani wala huwezi kusumbuka kuwatambua popote ulimwenguni.Basi wanyasa wanashughulika na mambo yao sasa kwani kale kalikizo kadogoka pasaka kamekwisha na inajionyesha watu wanarudi katika mstari wa kufanya kazi kwa bidii.Lakini jana kuna kina dada fulani walikuwa wakijimwaga mitaani kumalizia ngwe ya paska maana ni nyakati adimu sana kwa mtoto wa kike wa kinyasa kuachiwa huru kwani lazima afuate utaratibu wa kuishi kimila.ngoja nikomee hapa.

1 comment:

  1. markus mpangala06 April, 2008

    watu wanakula mahindi ya kuchoma,viazi,mihogo n.k yaani nyakati hizi ni vyakula vingi sana ambavyo najua dadangu huko ughaibuni anavikosa sana.kwanza anakumbuka mbelele?au kasahu kuwa hayo ni mambo yenye kipindi hiki?mandongo n.k

    ReplyDelete

Maoni yako