May 11, 2008

Monile,Inyahi na Eena Monile Za Wanyasa

Leo kuna jambo moja limenishtua lakini lilinikuna sana.Jambo lenyewe nilikwisha kuandika Bloguni hapa.Unakumbuka kile kisa cha Yasina?kisome.Basi leo tumewasiliana si unajua mambo ya simu ukiingia mjini wakati kwetu nyasa tunategemea barua enzi zile za Posta.Maana wahenga wanasema usidharau nazi embe tunda la msimu au huwezi kumkonyeza mtu kwenye giza.Najua dadangu kule ughaibuni akisoma atashangaa kusikia nimewasiliana na yule ninayemsimulia katika kisa kile cha hivi kwanini,visa vipo vingi nitakumegea rafiki wewe tulia tuliii kama maji ya mtungini,hapa nyasa tunaita "chihulu".Achana na hilo leo tazama kichwa cha habari hapo juu.Maneno hayo yanawakilisha salamu ukiwa hapa nyasa,ole wako usipoyajua...aaah natania tu....Ni maneno ambayo kila mgeni huwa mwepesi kuyatamka kwakuwa ni maneno yanayowakilisha mambo ya kila siku kwa Wanyasa.Yote yanamaanisha kusalimiana,kujuliana hali,afya,uzima,furaha,kujuana.kujenga urafiki,kupata mambo mapya n.k si unajua kumsalimia mtu unapata thawabu?.Lakini maneno hayo yamekuwa lulu kwa dada Janeti yule aliyetua nyasa akaanza salamu yake "inyahi".Basi kaongeza ujuzi wa lugha hii ya nyasa yaani nimeambiwa kwamba sasa ana kasi sana ya kujifunza mambo ya nyasa kwani yanamvutia na amependa sana nyasa.Hii yote ni kama nilivyosema wazazi wanapaswa kuwaeleza watoto wao wapi wametokea na utamaduni wake ili wajue.Sasa mama yake amekuwa Mwalimu wa lugha hii kwa dada Janeti yaani imekuwa lulu kwake kujifunza lugha hii "kilugha".Jamani nyasa ni mahali ambapo wakoloni waliishi na wanakumbukumbu nyingi tu hivyo mambo ya historia tunayo wala hatuhitaji kufika huko mjini kwenu maana nasikia eti kuna makumbusho ya taifa huko Dar es Salaam, Tanzania.Hivi hayo makumbusho ya wapwani ndiyo ya Taifa?Mnayajua makumbusho yanavyokuwa?Njooni nyasa muone,au unafikiri kwanini wageni wakija wanakunwa sana na maeneo haya.Ngoja nitaandika mengi ya kihistoria na kumbukumbu.Nakomea hapa au unataka niendelee kuandika.....sema mwenyewe kama unasoma halafu bado unatamani......niendelee?Eena Monile,Inyahi na Monile ujifunze kabla ya kuja nyasa ewe msomaji..nikuongezee mengine.......hapana dadangu kule www.ruhuwiko.blogspot.com ataongeza au umesahau?aisee tutagombana unabisha?aaah Natania tu

2 comments:

  1. Anonymous12 May, 2008

    eh monile numu,habari ja leleno kweli nimefurahi sana kwani kila nisomapo blogu zako nakumbuka sana nyasa. Nampa hongera sana mama janeti,kama hivyo na mimi nina kazi kubwa sana kuwa mwl wa lugha (kilugha) kwa watoto wangu. labda haitakuwa ngumu kwa vile tayari nimeshawapeleka kule nyasa na kuwaonyesha wapi nilizaliwa. Pia kuhusu Yasinta hivi kwa nini nimefurahi kuona mnawasiliana kwa simu kwani inaonekana mwisho utakuwa mzuri.Lakini hii imenipa shida kidogo kujua kama ni kweli Huyo ni yule Yasinta wa Mbinga au ni kinyume kwani hii habari imenipa utata kidogo. nitafurahi kusoma nini kinaendelea......

    ReplyDelete
  2. walongeza bwanji, habari j masova, habari ja leleno, gwali gwa mayahu na somba bwana wee

    ReplyDelete

Maoni yako