May 14, 2008
Ruvuma Yatolewa Kombe La Taifa,Huzuni...
Jana ilikuwa siku mbaya kwa Wanaruvuma shauri timu yetu ya soka katika michuano ya kombe la Taifa ilitolewa.Mechi ilikuwa kali bwana asikuambie mtu. kama hujashuhudia Wanaruvuma basi jinyonge kwa utandu wa buibui(natania).Nakwambia mechi zote za timu ya mkoa wa Ruvuma zinavutia sana,toka ile ya kwanza dhidi ya Kigoma.Basi jana mechi ikaanza mkoa wa Kagera kupata bao dakika ya pili kupitia kwa Musa Kaunda aliyemalizia pasi nzuri ya Shamte Ali.Lakini "wangoni" tukasawazisha katika dakika ya 34 kupitia kwa Abdalla Ausi ambaye alitumia makosa ya golikipa wa Kagera Odo Nombo aliyemrushia mpira huku akiwa ametoka golini.Katika kipindi hicho cha kwanza Pauli Ngwai aliipatia Kagera bao la pili baada ya kupata pasi ya Pauli Kabange.......mpira ukawa mapumziko.......Naam kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Ruvuma wakionekana kutafuta bao la kusawazisha.Kocha Pita Mhina wa Ruvuma alifanya mabadiliko yaliyosaidia kupatikana kwa bao la kusawazisha.Ruvuma walifanya shambulizi katika dakika ya 89 na beki mmoja wa Kagera aliutoa nje na kuwa kona ambayo ilipigwa vizuri lakini ikatolewa tena na kipa Odo Nombo,kisha mpira ukamkuta Omari Kapilima aliyeachia shuti kali lililokwenda kimiani.Lakini mnamo dakika ya 90 Kagera ilimwingiza golikipa Abdulrazak Jakisoni kuchukua nafasi ya Nombo, lengo lilikuwa kwa ajili ya penati.Mpaka Mwamuzi wa mchezo anapuliza kipenga(siyo kupenga kamasi) cha mwisho matokeo yalikuwa mabao 2-2.Sasa hatua za kupiga penati ziliwadia.Wafungaji wa Penati za kagera ni Daudi Chalesi,Martini Muganyizi,Juma Seifu na Ladislausi Mbodo.Zile za Ruvuma zilifungwa na Ramadhani Kudundwa na Patisoni Chiwanga ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi.Kiujumla Ruvuma walicheza vizuri na walipoteza penati mbili kupitia kwa Abdala Ausi na Daudi Ajilo....mchezo ulikuwa mzuri na kwa hakika licha ya kutolewa timu yetu ya mkoa wa Ruvuma ilicheza kandanda safi huku ikikusanya mashabiki wengi uwanjani hapo kuliko Kagera.Mchezo ulipendeza na dadangu pale bloguni ruhuwiko umeikosa mechi muhimu ya kuuona mkoa wako lakini najua ni majukumu tu.Tunahuzunika ....lakini tunafuraha timu yetu imecheza vizuri na ikitunzwa basi mwakani 2009 malengo yawe kufika nusu fainali kwani robo fainali ya mwaka huu inatosha Tuombe mungu kwa lugha yetu .....haya ewe mngoni na wengine anza.........mmh wavivu eeh..msijali mimi nimeiona mechi mnyasa mie yaani imenikuna sana....mmh nilisahau unajua huyu Odo Nombo kipa wa Kagera ni mtoto wetu wa Ruvuma?....unabisha?....Nimecheza naye Umiseta(michezo ya sekondari Tanzania) enzi zile na kina Masumbuko Hassani uwanja wa Majimaji pale,yaani kama siyo kuvua samaki hapa nyasa basi leo ningekuwa ughaibuni shauri ya kucheza soka tena kule Hispania shauri napenda sana soka lao maridadi halina fujo kama soka Uingereza wanaojisifu na........malizia wewe..
Madhumuni
kumbukumbu,
soka,
uzuri
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kweli kabisa tumwombe mungu Wanaruvuma wote. Nimefurahi kusikia kuwa wanaruvuma wamefikia hatua hiyo kwani ni mara chache sana kuona. Pia nasikitika hawaonyeshe mechi za huko nyumbani. (bahapo wangoni) angalao na sisi wanaruvuma tusonge mbele. Sasa kakangu hapo Nyasa kwa nini uliacha kucheza soka? aah lakini labda afadhali sasa wengine tusingepata hizi habari za Ruvuma kuwa inavuma. mie nilijua wanaitwa majimaji je wamebadili jina au?
ReplyDeleteNi kwamba mashindano haya ni ya kombe la Taifa siyo Ligi kuu,hivyo wanashiriki wachezaji wa mikoa yao waliyotokea.Majimaji imebaki kuwa klabu yaani timu ya mkoa ni kama timu ya taifa ya mkoa huo hukusanya wachezaji wa vilabu mbalimbali.Michuano ya mwaka huu inaonyeshwa na runinga ya ITV toka mechi ya kwanza,lakini pole najua huko ughaibuni huipati kabsia.Majimaji ipo haiwezi kufa ni mali ya wanaruvuma wote hekooooooooooo ayeyaaaaa
ReplyDeleteMmmh mdadisi dadangu!!Ni hivi nilikuwa mchezaji wa soka kiasi ambacho hata shule nisingeliweza kusoma,lakini kitu kikubwa ni kuumia goti la kushoto wakati wa umistashmta mwaka 1996 katika mchezo wa fainali.Nikaacha soka kwa muda lakini upendo wangu haukuondoka, nilirejea tena mwaka 2000 mwezi januari na mwezi Machi nikachaguliwa katika kikosi cha umiseta wilaya mbinga kisha mkoa Ruvuma kwani mguu ulikuwa umetulia haukuwa na maumivu kama awali.Jambo la msingi mama yangu hapendi wanawe tucheze soka na alikuwa akikasirika sana na kuombea tuumie ili tuache.Yeye alisisitiza kusoma.Lakini soka ni kipaji tulichorithi toka kwa baba yetu.Vilevile mdogo wangu yupo pale chuoni Nachingwea- Mtwara ni mchezaji anayeheshimika sana.Huyu mdogo wangu namkubali sana kwani anautajiri wa kucheza soka miguuni mwake lakini hajali kuhusu kipaji chake.Unajua napenda sana kucheza nafasi ya kiungo wa kati(namba sita)na kiungo wa kushambulia(namba nane) au kumi,pia beki wa kulia na beki wa kati namba nne au tano.kaka yetu naye ni mchezaji mahiri lakini hakuwahi kucheza kwa kuwakilisha wilaya ama mkoa kama mimi na mdogo wangu.Mpaka sasa naipenda sana ligi kuu ya Hispania kwani ina madoido sana ambayo nayapenda pia haiana kasi naiohsbikia kiasi Real Madrid.Mdogo wangu ni shabiki wa ligi kuu ya Uingereza ni mpenzi wa Manchester.Lakini siku hizi sipendi sana timu za ulaya napenda tiu yaetu ya taifa ya Tanzania
ReplyDelete