May 15, 2008

Kuzaliwa kwangu Na Teknolojia Mpya

Ndiyo leo ni siku yangu ya kuzaliwa.Nakumbuka miaka ile nilipozaliwa kijiji hiki cha Lundu hapa nyasa.Yaani naikumbuka siku maridadi.Sasa kuna kitu kimoja kinanishangaza sana,ni hiki kila ifikapo kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa nasahau kabisa shauri ya majukumu si unajua tena kuvua samaki,nyavu nazo zinahitaji tiba ikiwa zimeraruka.Lakini usiniulize wala usijiulize nimekumbukaje leo mpaka nikaadika.Tarehe hii ni muhimu sana Mama na Baba yangu ndiyo ilikuwa siku yao ya furaha kupata toto la kinyasa ambalo leo linapiga gumzo bloguni.Mmmh nakumbuka mwalimu wangu mmoja enzi zile alinifundisha eti kukumbuka siku hii ni sawa na kuomboleza msiba kwani mzazi wangu alipata uchungu sana...sawa ndiyo maana nawasifia kila dakika kwamba wazazi wangu ni zaidi ya upendo,kama unabisha soma pale bloguni pale ruhuwiko uone dada yetu alivyomthamini Mama lakini amemsahau Baba...sijui kwanini...ebu tuambie...Zawadi kubwa niliyojinunulia ni kitambaa cha mkononi(leso) chenye rangi ya bendera ya taifa ya Tanzania naipenda nchi yangu...Tuache hilo kwani tayari ni kumbukumbu inayonikuna.Kuna habari moja ya mambo ya teknolojia kwamba shirika la mradi wa Teknolojia la Tanzania(tzNiC0)limezindua mpango wa kubadili taarifa za mdalakilishi(intaneti)kwa lugha ya kiswahili.Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Beda Mutagahywa amesema hiyo itakuwa kama Google/wikipedia ya kiswahili ambayo itakuwa inataarifa mbalimbali za duniani kwa lugha ya kiswahili.Kasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya teknolojia TEKNOHAMA na kutoa mwaliko kwa vijana wenye uwezo wa kuandika taarifa waadnike humo zikiwa sahihi.Kwahiyo huu ni mwaliko kwa wanateknolojia....tunasubiri huku nyasa itatunufaisha hata kama hatuna umeme na mitandao

1 comment:

  1. Anonymous15 May, 2008

    eeh jamani samahani.Hongera sana kama watu wote wangefanya hivi kwa kweli wote wangekuwa na furaha sana pia wangekuwa wanakumbuka wana miaka mingapi.Nimefurahi kusoma kuwa umejinunulia zawadi leso ya bendera ya TZ kwa jinsi unavyoipenda nchi yako sawa bwana. Unazidi kuwatamanisha watu kwa kila njia wewe kijana ni mkali kweli. Na ni kweli inabidi uwashukuru sana baba na mama.KIla unapopata muda hata nusu dakika uwaombee kwa mungu.

    Yasinta ngonyani

    ReplyDelete

Maoni yako