May 27, 2008

Kumbukumbu,Kutoweka Kwa Rafiki Ya Baba Yangu

Jamani kama kuna kitu watu wanashindwa kukinunua hadi sasa.Unajua ni nini?Jibu furaha na huzuni.Hivi ni vitu ambavyo huwezi kununua popote na kama kuna mtu anauza hilo niambieni hakika nitajiua tena kujinyonga kwa utandu wa buibui wala usicheke.Nionyeshe nani anauza furaha na huzuni nimtunuku kifo changu hata kama ni mbele ya haki.OOH samahani sijaomba radhi kwanini nilitoweka hapa bloguni.Unajua majukumu mengine yalinibana yakanifanya nishindwe kuandika kuhusu wanyasa si unajua uvuvi samaki kunoga sana.Basi nilikuwa makini na usimamizi wa kumulika dagaa kitambo na ingawa tunasumbuana na mbalamwezi kwani dagaa tunawanasa kwa kutumia mwanga karabai na kutega nyavu na kuwavua hivyo mbalamwezi ukiwepo unaharibu mipango mutua ya kitoweo,mmenisamehe?aah sitorudia kosa nitatoa taarifa.Basi bwana furaha na huzuni ni hivi nimeuliza maduka yote hapa nyasa hayana, labda huko mjini mtanisaidia.Ni hivi leo nimewasiliana na dada yangu ambaye yupo makini sana na kazi zake yupo huko jijini Mbeya kwa Wanyakyusa.Huyu hana muda wa kupoteza mtoto wa nyasa,lakini usiniulize anafanya nini badala ya kuja kuchemsha dagaa,huo ni utaratibu tu.Mwisho ni huzuni,unaona sasa, pamoja na mikogo ya hapa na pale nina masikitiko/huzuni sana Rafiki ya Baba yangu amefariki.Ni habati ambayo nimeipata siku kama tano zilizopita.Nimeamua kumuenzi kwa kuandikia wanyasa wote kwamba Mzee Nchimbi Rafiki ya Baba yangu hatunaye.Mungu alitoa na mungu ametwaa,AMINA.kumbukumbu

2 comments:

  1. hizo dagaaa ningezipata ningejinoma kweli "ligwanda" tamu sana. eeh bwana we pole sana kwa niaba ya baba yako kwa kutowekwa kwa tariki yake.

    ReplyDelete
  2. Anonymous29 May, 2008

    Ooh. Ni kweli kabisa hakuna anayeweza kununua furaha au huzuni. Na pia ni hivi unapokuwa na furaha ni pale afya yako ni safi na una familia na marafiki ambao wanakujali. ni sawa na huzuni pia kwani kama unakuwa na rafiki ndugu na jamaa wakati wa furaha basi uwe pia wakati wa shida/huzuni.

    ReplyDelete

Maoni yako