June 02, 2008

Nyasa .....Hiyo usiulize Maswali picha itakasirika ..

Usiul;ize mnyasa vipi mbona kuna mtu hapo humtaji au hao huwataji?Mimi nakupa madoido ya Nyasa wala sitaki kelele.Mimi mtoto wa kinyasa utanimbia nini wakati najua utamu wa kuishi nyasa.Ngoja kwanza...jana kulikuwa na kichekesho eti jamaa alitaka kunitwanga ngumi wakati naadaa hizi picha,kisa eti wanyasa wanajiona matawi ya juu wakati hawana lolote.Mimi nikamwambia ingelikuwa hawana lolote basi wangelikuwa vichaa kwani mungu katuwekea kitu na tunacho nacho ni ubongo hivyo huwezi kumwambia mtu hana lolote kimaisha.Labda akifanya ujinga au kuleta ujivuni wakati hana ujuzi wa kile anachokisema au kukifanya.Yaani wapo watu ambao hawapendi kuheshimu wanachofanya wenzao hata kama ni jambo dogo....Nakwambia nilikasirika nikapiga ngumi kali ukutani lakini niliumia mpaka sasa nimefungwa bandeji nauugulia sana kisa kutetea wanyasa...njooni mnipe pole hata kuandika hapa natumia mkono mmoja tu wa kushoto......mbona hamnipi pole nanyi mna kisirani na wanyasa.....nitalianzisha varangati....ooooo ngoja nipone kwanza.

1 comment:

  1. Bahati yake mie nipo mbali kwani mie ndo ningemtoa meno yote angebaki kibogoyo. pole kwa maumivu ya mkonokwa niaba ya wanyasa wote.

    ReplyDelete

Maoni yako