June 02, 2008

Uoto wa Asili Nyasa Yetu...Karibu jionee

Angalia kunavyopendeza,angalia uoto wa asili,majengo ya asili.Lakini hapo ni makazi ya muda mfupi, unajua wanyasa huwa wanakwenda kuvua samaki mahli ambako hakujavulia siku nyingi?Basi wakifika huko hujenga nyumba kama hizo.Karibuni nyasa jamani yaani hapo tu sijawawekea wale wamisionari walioishi huku enzei zile za wale wahuni kutoka ulaya na wizi wao.Lakini kwetu walikuwa mapadre na mabruda.Mmh inanikumbusha nikiwa na ndoto ya kuwa Padre au bruda lakini samaki walinizidi kete wakanipa hamu ya kuvua.Muulize dada pale ruhuwiko{tafuta kwenye ukurasa wa Tovuti/blogu}bloguni akupe hamu ya wanyasa kuingi katika Monesteri za kijerumani..Mhh ngoja nikumegee msomaji unajua dadangu huyu alitaka kuwa nani?Utajiju nenda kaone pale Chipole misheni halafu utaniambia lakini usije ukanisingizia nimekwambia mimi..wala tena najificha uvunguni mwa kitanda...aaaah nimekumbuka kitu najua utasema mbona leo nina usongo wa kublogu...jibu sijaandika siku nyingi nimekuja na ari ya zamani,nguvu za zamani na kasi ya zamani.Naenda kula ugali na dagaa leo,tena jana jumapili nimekula

2 comments:

  1. Kwa kweli leo ndo umeniacha gizani kabisa. Umenikumbusha mbali sana yaani nilipomwona huyo samaki nikakimbia kuchukua ugali na kuanza kula eeh bwana we utamu wake sikuambii jaribu mwenyewe. Pia nimejikuta nipo Nyasa kabisa, nimepatwa na furaha ya ajabu mno kwa kweli jamani nyasa kuzuri. Umenifanya nikumbuke mengi kiasi kwamba natamani kurudi nyasa kwetu au unasemaje kwani tena nimetamani sana hao dagaa. Kwa kweli umefanya kazi nzuri sana. Swali moja je huyo ni samaki kutoka ziwa nyasa kweli au?

    ReplyDelete
  2. markus mpangala03 June, 2008

    Dadangu huyu ni mali yetu wanyasa kwa jina anaitwa LINGOMBOLI yaani ni samaki mjanja sana katika ziwa nyasa,havuliki kirahisi.Yaani anapendeza sana ukimwona mwenyewe.Yaani kila ninapomwona najihisi faraja kwani moja ya samaki ninao wapenda sana kuwaona,pia mwingine anaitwa Kanchungu huyu hapatikani kwa urahisi lakini yupo ziwa nyasa.Nimepata picha hii toka kwa wanyasa wa Malawi pale Monkey Bay yaani hawa ni wavuvi wenye ujuzi sana ndiyo walionitumia picha hizi.Hii ndiyo nyasa,huu ni mwanzo tu mengi yanakuja hasa nikiingia mwenyewe katika zana za kupiga picha muda mfupi ukao.

    ReplyDelete

Maoni yako