August 31, 2008

Ni kumbukumbu yangu leo nawapenda nyote

Nimetimiza mwaka mmoja tangu nilipoanza kuandika makala katika gazeti la RAI,ingawaje nilkitimiza mwaka mmoja mwezi aprili tangu nilipoanza kuandika makala lakini kwa hakika hili ni gzeti kubwa TZ kwahiyo kuadnika makala katika gazeti hili ni ndoto.Nilipenda kuandika katika gazeti hili wakati ule likiwa chini ya ninayemwita 'Mwanafalsafa' mze wangu Jenerali Ulimwengu,nina mpenda sana.Ingawa sasa anamekwisha kuanzisha gazeti lingine la Raia Mwema, soma www.raiamwema.co.tz bado naamini ipo siku nitafanya kazi na mzee huyu hakika nakipenda kichwa chake kina utajiri wa fikra. Najipongeza kwa kuwaambieni nawapenda nyote. Pia najipongeza tangu nilipoanzisha Blogu yangu,nayo leo nimetimiza mwaka mmoja sasa na kwa kiasa fulani inanipa moyo kwani nimepata marafiki wengi ambao wananishauri na tunawasiliana sana. Sina cha kuwaambia zaidi ya NAWAPENDA SANA,TUPO PAMOJA KAMA SAMAKI NA MAJI.
Amina, adumu sana ndugu yetu Ndesanjo Macha

1 comment:

  1. HONGERA HONGERA HONGERA sana Nimesoma baadhi ya makala yako kazi nzuri pia blog yako naipenda sana kwani ni wewe ndiye uliyenifanya nianze kublog. Kwa hiyo napenda kutoa pia shukurani za dhati na nakuombea kwa mungu akupe nguvu na moyo ili ufanikishe ndoto yako/zako. utafika tu.

    ReplyDelete

Maoni yako