September 25, 2008

kwa wanaotaka kwenda majuu


Usitoke katika nchi yako kama hujui unakokwenda. Huna mpango,hiyo ilikuwa moja ya nguzo zangu za kuandika TWENZETU ULAYA kuwaonya wenzangu kuondoka bila mpango
. Hayo ni maneno ya mzee wangu Fred Macha mtu ambaye sikosi kusoma kazi zake iwe katika magazeti au vitabu. Vijana wengi Bongo tuna ndoto za kwenda Ulaya,lakini nami nawaonya ikiwa umeshindwa kuweka maisha yako vizuri hapa basi usitajie kufanya hivyo ughaibuni,wengi wanadanyika na picha z akwenye filamu na majumba makubwa kana kwamba ughaibuni kuna mazuri zaidi. Lakini hatujiulizi haya mazuri yanakujaje. Enyi wenye ndoto za mchana kwamba mnakwenda ughaibuni kusoma,hivi manajua kwa undani nini kinachofanyaika katika za wenzenu? hivi digrii tu mtu anaitafuta ughaibuni wakati tuna vyuo vingi hapa Tanzania. Tena ni afadhali ukaenda nchi zilizopo ndani ya bara la Afrika kwwani zinafanana isipokuwa Afrika kusini ambako mambo ni kama huko ulaya. Tafuteni kitabu cha MPE MANENO YAKE kilichoandikwa na mzee huyu kwani ni mkusanyiko wa mambo yaliyotokea mahali alimoishi. au soma mohajiano/habari nzima hapa; bongocelebrity.com/.../kwa-kina-na-freddy-macha

4 comments:

  1. hahahahaha Ughaibuni. ndugu zangu sikieni jina tu ughaibuni. Msidhani ya kwamba nawatisha hapana, ughaibuni kuna shida zake ambazo afadhali hata ya Afrika yetu. Kuwa na jumbe, pesa, gari elimu nk sio kitu kama huna marafiki au wapo lakini hawana uchangamfu sio kama waafrika. Nawaambia kama kuna mtu anataka kwenda ulaya haya lakini Afrika ni namba moja kwani nimewasikia wengi ambao si waafrika wanasema mimi nikiwa mzee nitahamia Afrika.

    ReplyDelete
  2. Hivi kwa nini watu wanahama kwao? Hii tabia inahitaji kufanyiwa utafiti wakila kujua kulikoni. Maana ambao hawajahama, wanaota kuhama. Waliohama, hawarudi. Kinachowakimbiza ni nini? Umasikini? Kama ndio wenyewe kwani haiwezekani kupambana nao tukiwa humu humu? Mentality mbovu sana hii.

    Kazi za Macha nazipenda. Mimi huwa nanunua mwananchi kwa sababu ya hadithi zake. Ana staili flani ya tofauti.

    Kazi nzuri kaka. Nimependa blogu yako.

    ReplyDelete
  3. Hivi kwa nini watu wanahama kwao? Hii tabia inahitaji kufanyiwa utafiti wakila kujua kulikoni. Maana ambao hawajahama, wanaota kuhama. Waliohama, hawarudi. Kinachowakimbiza ni nini? Umasikini? Kama ndio wenyewe kwani haiwezekani kupambana nao tukiwa humu humu? Mentality mbovu sana hii.

    Kazi za Macha nazipenda. Mimi huwa nanunua mwananchi kwa sababu ya hadithi zake. Ana staili flani ya tofauti.

    Kazi nzuri kaka. Nimependa blogu yako.

    ReplyDelete
  4. hahaha,ulaya hakuna kitu maisha yanabana sana,hakuna amani ya rohoni kila wakati mtu upo tu afadhali ya jana.Mimi nina rafiki zangu kadhaa wa kizungu wamechoka na maisha ya ulaya na wameniomba niwatafutie sehemu za kuishi tanzania,kwani wanafikiria ulaya sio sehemu ya kuishi,sasa wenyewe wanaondoka je wewe utapaweza?

    ReplyDelete

Maoni yako