October 18, 2008

mume+mke = papo kwa papo

NA JOYCE JOLIGA, SONGEA
Ni kamba serikali ya halmashauri ya mkoa wa Ruvuma inajenga wodi ya uzazi(upasuaji. Wazazi wengi walikuwa wakijifungua katika chumba maalum na kurejeshwa katika wodi ya akina mama ambayo ilikuwa na kero nyingi. Lakini ufumbuzi huo umepatikana na waume zao wakuwa bega kwa bega katika kujifungua kwa wake zao. Hivyo kusudio hilo linafanyika baada ya kuona usumbufu wanaoupata akina mama kwa kujifungua. Waume watatakiwa kuwa karibu na wake zao hasa wale wanaopata uapsuaji wa uzazi/kujifungua kwa njia ya kupasuliwa. Maana yake sasa wanaume kushuhudia namna wake zao wanavyojifungua? Hapana bali ni kuwa karibu na wake zao hao baada ya kufanyiwa upasuaji.

NA HAPPY KULANGA, SONGEA
Wakulima wametakiwa kujiunga katika vyma vya ushirika ili kupata urahisi wa kununua matrekta madogo ya kulimia ili kuongeza tija katika sekta ya kilimo. Mkuu wa mkoa amewataka wakulima kufanya hivyo ili kuweka mazingira mazuri ya uzalishaji.

NB; unatakla kuwekeza katika Mkoa wa Ruvuma? Njoo wekeza ufaidike sasa usingoje

3 comments:

  1. Nimefurahi sana kwa jambo hilo kwani ni muhimu sana wanaume nao wajue ni kazi gani mkewe anaifanya. Na ningefurahi zaidi kama wenaume wakikuwa katika chumba cha kujifungua kwa njia ya kawaida muda wote tangu mwanzo mpaka mwisho. Kwani kuna mafundisho mengi. Ngoja niende nikawaambie jambo hilo

    ReplyDelete
  2. mm tafadhali usifanye hivyo, napiga magotiiiiii tafadhali usiende kuwaambia

    ReplyDelete
  3. hakuna cha magoti nakwenda kwani hapa tayari nimeshafunga begi. inabidi mjue

    ReplyDelete

Maoni yako