December 08, 2008

aaaah!! nina HAMU !!!

Nina hamu sana unajua? Nina hamu ndiyo maana nakwambia nina hamu mpaka nashindwa kujizuia. Nina hamu mpaka nataka kulia. Si hamu nyingine bali ya kukusalimia MAMBO? aaaaaah umnielewa huna hamu ya DAGAA wewe?

5 comments:

  1. aaha wenga ndawa ya kiki ukita naaa sipa ogo na muyako ukuninogesa kweli. mwenga mbona gwali gwene kudebe

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa lugha hapo juu, lakini nahisi da Yasinta kahadaika sana kuona dagaa. Hak'ya Mungu mnanikumbusha wakati nikisoma Kigonsera, walikuwa wakilowekwa tu na kuletwa bwaloni tule, niliwachukia sana.
    Lakini huwezi amini, leo hii ni mboga niipendayo sana. Huku Daslamu ikiwa imeungwa kwa nazi, na mahanjumati mengine kidogo, halafu ugali ama ubeche, da Yasinta utasahau hata kwenu Peramiho.
    Markus kaka, utantia wazimu,
    dagaa wanipa hamu,
    ni chakula kitamu.
    Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  3. umeelewa vizuri tu Fadhy, yaani hapo amenipa kichaa mno amenipa hamu kiasi kwamba natamani kulia dagaa nyasa basi tu. Ni tabia mbaya sana kutamanisha watu hivi. kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  4. Sijui inakuwaje mtu mwenye hamu anapokuwa na alicho na hamu nacho na kuanza kuwaringishia wale ambao pengine wanajua itawachukua mwaka na zaidi kukamilisha hamu yao. Sijui nikulaumu kwa kututamanisha ama nikupongeze kwa kutukumbusha? Ntachukua njia sahihi. Ntakupongeza Kaka. Umenikumbusha namna ya kuwatunza dagaa ukinunua wengi, na namna ya kuwapika wakiwa wabichi. Umenikumbusha ladha ya chakula kimojawapo chenye lishe bora na kitamu sana. Kaka Markus, UMENIKUMBUSHA NYUMBANI na kwa sasa sina hamu ya kusema MAMBO!, nina hamu na nyumbani.
    Blessings

    ReplyDelete
  5. Najua una HAMU ndiyo maana umesema. najua HAMU ni nzuri kwani inajionyesha bila kuongea. ha ha ha ha Poa kaka Mzee wa changamoto haya ndiyo mambo ya nyasa mkuu ni utamu na hamu tu. karibuni tena na tena maana RUHUWIKO pale ni mishikaki sana ya kitimoto kwahiyo sisi tunakuletea dagaa tu ujing'ateng'ate kwa HAMU.

    ReplyDelete

Maoni yako