December 24, 2008
waambie ROHO yangu nzuri, AMA ZANGU AMA ZAO
nashangaa wananichukia bila sababu, sijawatendea madhambi lakini wananitumia ujumbe wa simu wataniua, eeeh ongezeni juhudi sitoacha kundika kile ninacho amini tena mimi mfuasi wa MALCOM X, kwangu Martin Luther King jr siyo shujaa! naamini hivyo licha ya kukubali umahiri wake, napenda ukali wa X kwani unaonyesha msimamo siyo kupewa sifa za upole na ustaarabu, waambie ROHO ni nzuri kuliko picha. Sijawatendea madhambi nashangaa wana chuki, wanataka kunihukumu, wamefanya kikao cha kumaliza roho yangu, nasema niueni anza hata sasa mimi sitishwi kwa ujumbe mfupi wa maneno ya simu eti sitowezi kuzuia kifo, eti wataniua kwsababu zao sijui nilichowakosea lakini SITISHWI na mtu yeyote wambie AMA ZANGU AMA ZAO hiki ni kima changu ama chao iwe mtaani maskani au mahali popote pale, kwani dunia nzuri kama picha hii hutoa taswira upendo na nafasi zetu. Waambie upendo wangu haupo kwa maadui, ndiyo kwani naogopa KUFA labda sijazaliwa waambie tena na tena ukiona uzuri na upole wa picha hii utadhani hakuna SHARI. Anzeni basi, kwani HATARI KITU GANI?
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ninaamini nimeweza kugundua falsafa ya maneno haya. Ama zetu ama zao. Naomba nisiandike zaidi nisije nikaharibu zaidi.
ReplyDeleteMkuu hii ilinishangaza sana lakini kwakuwa dawa ya jeuri ni KIBURI, nikaamua kuandika hapa ili kichwa kipoe kwanza. Maana niwazapo zaidi nahisi nimevaa nasaba za MALCOM X. jamaa wametuma sms mbili 24/12/2008 saa kumi jioni, wakitamka neno kifo kwangu siwezi kuzuia, wanasema hili ni jambo ambalo kila binadamu ameshindwa, na kifo changu kitatokea tokana na mazingira. Nilicheka sana maana anayetaka kukudhuru hawezi kukuogopesha yeye hutenda tu halafu unang'amua baadaye kwamba aaalaah kumbe jamaa alipanga kitambo. Lakini hawawezi kuzuia mvua, hiki ni kiama changu ama chao, iwe mtaani maskani au mahali popote pale amiri jeshi mkuu sasa nimekwisha tangaza vita maana watoto mama wanachonga sana, kelele kibao kunitishia kifo! maisha yangu siogopi kufa ndiyo maana siamini kuwa habari za mungu au imani lazima uwe na dini. Yaaap mkuu Bwaya. Pamoja daima
ReplyDeleteDUH!:-(
ReplyDeletehii inakuwaje tena mwanawane, mbona hatujuzani ni akina nani
ReplyDeleteKaka Mpangala, ukiona hivo basi ujue ushawazidi kete hivo wanafanya danganya toto ili usikaze buti...
ReplyDeleteKuna watu wapo bega kwa bega nawe