Jana nilikuwa nasumbuliwa na swali hilo hapo. Nilikuwa nawaza mengi sana kuhusu binadamu kulia. Nimejaribu kuatafuta vyanzo nakuta ni kama vile MAKOSA, HUZUNI, FURAHA na mengineyo ambayo hayael;ezeki.
Ninajaribu kufikiria sana suala hilo ingawaje naona kwa wtoto ni jambo ambalo limekuwa katika eneo la makuzi yetu. Je nasi tunapolia tunatoa ishara kwamba hatujakua kwahiyo tunahitajika kukua?
Nawaza suala hili haya jawabu nakosa...na wakati mwingine nimewauliza wadogo au watu wazima naona jawabu lao ni moja eti kawaida. Najiuliza ingekuwaje pasingekuwepo na kulia? Nimeuliza hivi wewe Mume wako amefariki, na unajua hataweza kurejea tena kwani unalia? Nini kinachokuliaza hasa?
Wewew umemkosea mtu jambo lolote, na unajaribu kumwomba msamaha, eti huku unalia na kuangusha mchozi, kuna uhusiano gani kati ya kulia na makosa yako>? Iwapoumemkosea rafikiyo, ndugu au wazazi kwanini unalia? Kuna siri gani katika kulia kwetu wandamua
No comments:
Post a Comment
Maoni yako