November 27, 2009

ALIKUFA MWAKA 1995, AKAONEKANA MWAKA 1998

Kwetu Nyasa suala la uchwai ni jambo ambalo kila familia inafahamu. Na hilo limekuwa likitendeka katika mambo mbalimbali ikiwemo ndani ya ziwa nyasa. NGOJA NIKUSIMULIE HIKI KIOJA KILICHOJIRI PALE KIJIJI CHA chinula kilometa kadhaa kutoka Mbamba bay.+++++++++++++++++++++++

NI Mwaka 1995 Romwadi(siyo jina sahihi) alifariki dunia kwa kutumbukia ndani ya ziwa nyasa,. Romwadi alikuwa akitoka kutega nyavu zake kama ilivyo kwa wavuvi wengine. Alikuwa mchangamfu na mwenye kila ina ya furaha kwa matarajio kuwa sijku inayofauata angelipa kitoweo kizuri.

Furaha yake ilitokana na kile alichoamini kuwa nyavu zake ni mahiri sana, kwani zimekarabaitiwa na anauhakika wa kuvua samaki wengi. Hii ilikuwa kawaida yake kila ategapo nyavu zake hunasa samaki wengi sana kiasi ambacho wengi humuonea wivu. Romwadi aliendelea na tabia ya uvuvi wenye tija kwani maneno ya watu hayamkumfanya asitishe kazi yake. Alijua wivu wao unatokana na jitihada zake alizofunsishwa na baba yake ambaye alimwamini kwa kila jambo.

Awali Romwadi alidhani kelele hizo za kutaka kukagua nyavu zake aliweka nini hata samaki wakawa wananaswa wengi zilimkasirisha siku moja tu, na siku ambayo ndiyo ulikuwa mwanzo wa uhasma wake na baadhi ya wavuvi. Wengi walidhani kukasirika kwa Romwadi kulitokana na jeuri ya kuvua samaki wengi kuliko wengine. Alijua huo utakuwa mwisho wa wale wanaodhani anatumia dawa zozote kuvua samaki.

Pamoja na hayo, Romwadi alivumilia na kuamini kuwa uhasama huo ulikwisha kwani haukuwa na tija kwake wala kwa wavuvi wenzake. Aliamua kuendeleza jitihada zake za uvuvi huku baba yake akimwambia anatakiwa kuwa mkimya pale watu wanapomkosoa kuhusu umahiri wake wa kuvua samaki. Zamani aliona ni jambo la kawaida sana, hata akamua kumwuliza baba yake kuwa kwani watu hawa wanamsakama wakati ni mungu aliyeweka samaki hao? Baba yake alimweleza kuwa hakuna jambo bora kama ukimya kwahiyo yeye aendeleze tu juhudiza kuvua samaki.

Bila kuelewa nini kinafuatia siku ya Julai 14/1995, Romwadi aliamua kwenda ziwani kama ilivyo kawaida yake, akaamua kuchukua mtumbwi wake na kwenda kilindini kutoa nyavu zake. Asubuhi ile alikuwa akijaribu kuonyesha tabasamu kwa wenzake kwa madai haukuna jambo baya miongoni mwao na kati yake. Alikwenda kilindini, akapata samaki wengi sana, akarejea nao nchi kavu kama kawaida ili awatoe na kwenda zake nyumbani. Jitihada hizo zilianza kutoa machungu kwa Romwadi kwani alipofika tu nchi kavu wale wavuvi wenzake wakaanza kumshambulia kwa maneneo baada ya kuona idadi ya samaki aliopata.

Hakuwa na jawabu kwa mtu, alikumbguka maneno ya baba yake kuwa anatakiwa kuwa mpole kwa kila jambo ambalo linaweza kuleta uhasama na kuathiri maisha yake. Mchana ule akiwa nyumbani akipumzika na kungojea muda wa kwenda ziowani akatege tena samaki wake, alijiona kama mtu mwenye kitu kooni lakini hakujua ni nini hasa kilikuwa kikimkwaza wakati huo.

Alimweleza baba yake, lakini baba huyo alimjibu kuwa aachane na mawazo ya wavuvi wale kwani atakuwa akikwazika mara nyingi. Baba yake alijaribu kumwelimisha kuhusu umuhimu wa kuskiliza watu wasemacho wakati ukweli anao, alimweleza hakuna kitu kibaya kama ugomvi kwa wavuvi wa bandari moja kwani inaleta uharibu miongoni mwao. Romwadi alikuwa mtiifu, akatii matakwa ya baba yake. Tokana na upole wake wakadhani hawezi kuwajibu lolote baya wasilotegemea.

Jioni ilipowasili siku hiyo, alikuwa ameambatana na nduguye mmoja ambaye alikuwa akimdadisi siri ya kuwa mkiywa sna siku hiyo, lakini Romwadi alimwambia ndugu yake kuwa hakuna lolote baya bali ameamua tu kuwa mpole. Wakati akiondoka hapo nyumba alimweleza baba yake kuwa haoni kama wataonana kwani anahisi kuna kitu kitatukia huko bandarini. Lakini mzee wake alimwambia hakuna baya lolote.

Laiti kama Romwadi angelitambua kuwa hiyo ni siku yake ya mwisho katika uso wa dunia hususani kijiji cha Chinula, basi asingelikwenda kule ziwani/bandarini kwaajili ya kutega nyavu zake. Alipofika bandarini alipakia nyavu kama kawaida, na akaondoka kwenda zake kwenda kutega nyavu hizo, LAKINI kabla hajamailiza kuzitega alikumbwa na kizunguzungu, ikabidi nduguye amsaidie kumpepea, ndipo akapata nafuu.

Sekunde kumi baadaye alimweleza ndugu yake kuwa anaona watu wanacheka wanamwita huku wakimwonyesha sehemu asiyoijua, lakini nduguye alimwonya kuwa hakuna kitu kama hicho kwani wakati huo ilikuwa yapata saa 10 jioni. Kbala hata nduguye hajapata nafasi ya kunena tena, akashangazwa na kauli ya ndugue kuwa, TUTAONA MUNGU AKIPENDA. Hiyo ilikuwa huku akitumbukia ndani ya maji kwa kusukwasukwa na wimbi dogo sasna ambalo halikuwa na uwezo wa kutingisha mtumbwi. Romwadi akapotea ndani ya maji kwenye kina kirefu. Hakuonekana tena.

Katika jitihada za kumtafuta, haikusaidia lolote, Romwadi hakuonekana-AKATANGAZWA AMEKUFA hiyo baada ya siku tatu za msako, msako ambao uliwakusanya wazamiaji wote wa samaki wa pale Mbamba bay, walikusanyika watu kadhaa pale kijiji cha chinula, lakini hakuna kitu kilichobadilika, Romwadi hakuonekana. Ikawa tu wakaanza kulia na kutanga msiba mzito katika familia. Baba yake alikataa kunyoa nywele zake kama ilivyo ada kwa waafrika misibani. Alisema hatanyoa nywele za ke kwani mwane yuko hai na mungu atamlinda tu.

Mkwa1996 ukajongoea, ukaihsi na ukaishia Romwadi hakuonekana. Lakini mwaka 1997, alionekana katika nyuma ya mlima Mbamba bay ambako kuna pori kubwa lenye msitu wa kutisha . Msitu ambao wengi hawathubutu kwenda peke yao.Waliomwona walishanganzwa na uwepo wake. JE walimwonaje? Akinja ama kama kawaida yao walikuwa katika harakati za kutafuta Likungu mboga adimu sana hapa nyasa. Wakiwa na vikapu vyao wakijiandaa kukapa likungu hilo waliona mtu mwenye nywele ndefu na ndevu za kutisha huku sura yake ikionekana kwa mbali.

Akina ama wale walitaka kuondoka lakini walishangaa mtu huyo mwenye nywele ndefu anajongea walipo kwani aliwapa ishara ya kutoogopa. Hamadi... alipfika jirani tu mmoja wa wale wakina ama alimtambua... akashangazwa na uwepo wake.... akajaribu kumsemesha lakini Romwadi ahkuweza kuongea. Hadi hapo akina ma wale walitambua huyo ndie kijana Romwadi aliyepotea katika mazingira tatanishi katika kijiji cha Chinula.

Wakaanza kuhangaika lakini kijana Romwadi aliwaonyesha ishara nyingine kuwa wasikimbie... akawaambia kwa ishara kuwa njaa inamuuma hivyo anahitaji msaada. Wale akina mama walishindwa kumsaidia zaidi ya likundu alipobeba. Wakampatia akala kwa harara... akawaambia kwa ishara waende kwa baba yake wamweleze yuko hai lakini hawezi kuonmgea.

Akina mamma wale walipoondoka tu ndipo sekeseke ikaanza kwa kijana Romwadi kuugua kifafa kila mara mara, akawa ameanguka mara nyingi na kuchubuka sehemu mbalimbali za mwili. Hata sura yake ikaanza kubadilika kutokna na makovu hayo.+++++++++++++++ huku nyumbani akina ma wale walifikisha taarifa kituo cha polisi Mbamba bay, pia taarifa zikafikishwa hadi kwa baba yake.. ndipo kundi likaotoka huku kwenda kumsaka Romwadi.

Polisi walijiandaa vema, wakaungana na akina mama wale hadi kuho nyuma ya ule mlima(mtaa wa zambia), lakini walifika eneo walilomwacha hawakuona kitu, wakasonga mbele zaidi...ghafala wakashangazwa na kicheko cha mtu aliyekuwa juu ya mti, wote wakaangaza huko na kuona kijana Romwadi akicheka na kuwashangaa viumbe hao. Baba yake alimtambua mwane...lakini hakuweza kumshawishi ashuke mtini. Lakini akaina mama wale walipomwambia kwa ishara ashuke...akaanza kushuka taratibu....bila kutegemea akatoweka mbele ya nyuso zao, wasione tena kiwiliwili cha Romwadi wala kusikia sauti yake. IKAWA AMETOWEKA.


Mwaka 1998 akadaiwa ameonekana maeneo ya umatengoni katika kijiji cha mpepai, akilima kahawa na wengine. Huku akiwa na nywele nyingi kuliko wengine. Ikadaiwa kati ya wachawi hao walipeleka taarifa kwa baba ayake ambaye alishangazwa na habari hizo. Akataka kufautilia, lakini kabala hajafanya hivyo akapewa taarfia na wachuuzi fulani waliopita hapo kijiji cha Chinula na kuhadithia habari za Romwadi.

Wakasema ni kijan mchafu, analima kila siku bila kula, na kuna watu wanafanyisha kazi hizo kwani wlaimnunu toka kwa wacahwi wa nyasa. Hbari hizo zikafika polisi lakini kabala hawachukua hatua kijana Romwadi akaonekana katika kijiji cha LINDA kilometa kdhaa kutoka Mbamba bay. Huko alikamatwa na baadhi ya vijana walioamua kumtia nguvuni ili kunusuru maisha yake. Na walifanya hivyo ili kushinda na nguvu za uchawi zilizokuwa zkimsumbua. Ghafla akatoweka katika mikono yao. Ilikuwa halai ya kutisha laiini baadhi ya wachawi wa maeneo hayo walidai wanashinda kwani hawataki kumwachia kwani anatakiwa anendelee kulima.

Punde polisi walipofikia kijiji cha Linda, wakafanikiwa kuongea na wazee wa mji na kuwaambia umuhimu wa kumrejesha nyumbani kijana huyo,....na wale wazee wakataja wachawi wanaomchezea kijana huyo kama taahira. Ndipo ghafla kijana Romwadi akaonekana ameketi bara barabarani, huku akiimbna nyimba zisizo na maneno. Polisi wakamchukua wakampeleka eneo salama katika ulinzi na kumwiata baba yake ili amtambue. Mara baba yake alipofika alimtambua kuwa ndiye mwanaye aliyefanyiwa mazingara kwa kutokweka kwa kuangukia ndani ya maji ziwani kisha kuonekana nchi kavu akiwa hai.

Akatafutwa mganga toka malawi ambaye ndiye aliyfanikisha kumfanya Romwadi ataje mahali alipoishi na wale waliokuwa wakimtesha na kumfanyisha kazi nyingi. Romwadi alifanyiwa usafi na kurejeshwa nyumbani chini ya ulinzi wa polisi. Kumbuka hakuweza kuongea hadi jitihada za mganga huyo.... aliposema kuwa nahakika ataongea na kweli akafanikiwa kuongea..
Hiyo mwaka 1998 akawa amerejea kijijini kwake huku akishangaa nguvu za wachawi. J E UCHAWI UPO AU HAUPO?

NB nina visa vingi vya aina hiyo, lakini swali linabaki kama UCHAWI UPO AU HAUPO. KAZI KWAKO MSOMAJI NAHITAJI MAONI YAKO.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako