November 24, 2009

KATIKATI YA MAELEZO, KUNA SWALI

Sina cha kuandika leo ingawaje naandika. Lakini ninachoanadika ndicho nisichokifikiria lakini naona tu maneno yanatiririka kama maji mtoni. Nakumbuka nilipoanza kuwaza sikupata jawabu kama nawaza lakini sijui nakumbuka nini.

Nasikiliza maenelezo mengi tu, nayaona na kuyasoma mengi lakini naongea machache sana yenye mkondo mmoja tu ambayo ni mahusiano ya sisi wanadamu. Sasa wakati maelezo yanatoka nikajikuta nina ninaswali ambalo linatakiwa kujibiwa mwishono na nikajua sitajibiwa katikati ya ya maelezo.... duh! sijachanganyikiwa ila najikuta naandika tu sijui nawaza nini...hebu msomaji nisaidie katikati ya maelezo yangu kuna swali...na pengine kuhusu utashi wangi wangu.

Acha bwana mawazo mengine hata hayana huruma eti yanakuja tu na kujiwazisha yenyewe kama yalivyo. Na nadhani nawaza kwasababu tu ninakichwa chenye kiwazua mambo lakini sifuri kabisa hakina ustaarabu. Na inatosha tu kusema sijui nawaza nini.....

Nimekumbuka msimu wa kuogelea unavyoshamiri nyasa sasa, watu wanajiandaa mwisho wa mwka kwenda kujiburudisha huko jamani sijui vipi wasijua kuogelea aibu yao ........nina uhakika hata wewe msomaji hujui kuogelea, njoo nimeanza kufundisha namna ya kuogelea vizuri lakini usije na masharti nisikushike popote aiseh..... SINA KITU leo ndiyo maana napumzika tu kwa kuandika hivi......

Ngoja nimsikilize kipenzi changu King Gk anipoze na mistari ya kiHIP HOP yenye majigambo kinamna au siyo msomaji wangu.... nachagua kibao bomba sana SAUTI YA MANKA. haya anza .....

No comments:

Post a Comment

Maoni yako