July 12, 2010

Wooh!! PALEPALE PALIPOUNGUA SHOKA NA MPINI UKABAKIA.........

Kama kuna kitu ambacho unakipenda halafu ukajikuta hutakiwi kukikosa utafanyaje jamani? Eti kuna umuhimu wa kususa kitu unachokipenda kweli? Au heshima unayompatia mtu inatakiwa iweje jamani? Maana mimi huwa naheshimu ninachokipenda na huwa natekeleza haswa. Mfano huu mpira uliokwisja jana hapa na kuona wachawi wanaowanga na nyungo kwa kutumia Pweza wametabiri mambo halafu wanaita utabiri wa kiteknolojia. Duh! ingekuwa afrika eti utamaduni wa kishenzi..... ha ha ha Nanyi ushenzi wenu ukae wapi jamani wazungu ninyi? Samahani kwa MCHARUKO huo.

Kombe limeisha, sasa nimerudi jamani yaani kikamilifu kidogo maana kuna mambo yanatakiwa yakamilike mwezi huu wote ndipo nitasema kweli kombe limekwisha sasa. Yaani RAHA kweli namshangaa rafiki yangu Yasinta anaangalia mpira kwa 'kubip' yaani haangalii kwa undani na umakini yeye anacheki kidogo na kuendelea na mengi Lol.... nitakucharikia aaaaah kumbe Erik amechukua tabia zako kidogo afadhali hii hajachukua mweeeee! WADAU wangu nimerudi,

WADAU wangu pale MKWAWA UNIVERSTY Francis Myale, Castro Tunuka na yoo man Jose a.k.a Jose, nimeipata barua pepe yako nitakupaisha mwana. Nilikuwa bizie na hii mipira ya JABULANI na mdogo wangu na rafiki yangu  Elvis Msigwa, utamwambia nini kuhusu soka huyu? Aaah mpira bwana mtamu usifananishe bwana. Yaani weka mahaba kando kabisa..... Mtani Fadhy a.k.a shemeji aaaaah ulipendeza kaptura lako a.k.a pensi naona shemeji anakaangiza kwelikweli yaani we acha tu. Kama kawaida Papaaa  yaani palipo ungua shoka na pini ukabakia........ PAMOKA DAIMA ++

2 comments:

  1. Anonymous12 July, 2010

    Ha ha ha haaaaaaaaa.....shemeji huo sasa utani. Unajua hili joto la Dasilamu si vibaya mara moja moja tukatinga pensi. Zamani kulikuwa na pensi nyanya...

    Kombe la dunia limekwisha. Karibu pale mwanachi mimi kuna waraka wa Mtume Fadhy

    ReplyDelete
  2. nanukuu "Aaah mpira bwana mtamu usifananishe bwana. Yaani weka mahaba kando kabisa..... " mwisho wa kunukuu hapa nde nihekili kweli mdala waku alapata taabu yididi mlondayi mwe igana kulola mpira ngati veve.

    ReplyDelete

Maoni yako