July 17, 2010

NIKUPE NINI?

Nikupe nini ewe rafiki? Nifanye nini kwako rafiki mwema, usiyeficha msimamo wako na kukataa kile kisichokuwa chema? hakika wajua thamani ya urafiki, wajua thamani ya ukweli na upendo kwangu, Nitakupa nini rafiki yangu? Mangapi yangu yamesemwa na ukaambiwa lakini hujanificha?

Nifanye nini maana bado najiuliza kila siku? Najua tumetofautiana mara kadhaa lakini uzuri tunajadili yanakwisha. Najua habari kadhaa zangu umezipata na pengine unashindwa kunielewa misimamo yangu kadhaa. Lakini uzuri wajua tabia,mwenendo,misimamo,mitazamo na hadidu zangu za rejea.

NIKUPE nini ewe rafiki yangu? Sema sasa nijuwe maana kusubiri nishachoka nisije nikawa MVUMILIVU HULA MBOVU. Wajua ni kwanini tumekuwa hivi, wajua ni ukweli,bila simanzi, ni upendo na uwazi. Aaah! nitakupa nini ewe mwema. Naamini mungu ajua yakuwa twajua kwamba kiasi cha mambo tuyajuayo ni sehemu ya kujua tu ingawa pia hakutoshi kuyajua.

Asante rafiki kujibu hata maswali yaelekezwayo kwako lakini yanihusu mimi. Yote tisa naweza kukuita hakimu mzuri kwa kuhukumu vizuri  bila upendeleo Lol.... You know what it is rafiki. Daima umesimamia ukweli. Nakupenda sana rafiki yangu. Hivi ni nani atakaye tutenganisha? au huyu Mungu? ataweza kweli maana ananiogopa kila siku...... Lol

Napenda staili ya urafiki wetu mama, naamini ni ndugu sana kwa mengi mema. Zaidi nimeipenda picha inanikuna sana. JE URAFIKI UNASOMEWA DARASANI AU CHUO KIKUU? Thamani yeru ya urafiki ni pale tunapotazamwa kwa tofauti kumbe walaaaaaaa! Mungu mkubwa! THE SAME DRAMA

6 comments:

 1. Zawadi kubwa unayoweza kumpa rafiki ni kumkumbuka katika sala zako.

  ReplyDelete
 2. kwanza nasema ahsante sana. Pili nasema huhitaji kunipa kitu unachohitaji kusema kwangu ni AHSANTE TU!!Kwani leo umenikumbuka hii ni zawadi nzuri nami nasema ahsante sana.

  ReplyDelete
 3. Pia kumtembelea rafiki huyo ni jambo jema litakaloimarisha urafiki wenu....LOL

  ReplyDelete
 4. Anonymous21 July, 2010

  huyo anakutaka yasinta anashindwa kusema ndio anaanzia mbali

  ReplyDelete
 5. Nawashukuru nyooooteeeeee.
  @Kaluse; kumtembelea siyo jambo gumu ni maamuzi tu. Nikunong'oneze. Unajua kisa ya safari yake ya pili kurejea bongo hadi ruhuwiko????? ha ha ha ndiyo hayo nasema muwe mnauliza! Lol ha ha ha MCHARUKO huooooooo.

  ANON @julai 21. ama kweli wivu humuua mtu mjinga. IWEJE UMPENDE MUNGU USIYEMUONA, NA UMCHUKIE BINADAMU UNAYEMUONA???? Mcharuko.
  Nakupongeza wewe ANON kwa mawazo yako mazuri ILA nakushauri uwe unaisoma hii blog toka ilivyoanza 2007 agosti utakuta habari nyingi za Yasinta rafiki yangu. kwahiyo sijui utasemaje.
  WAZO TU, nadhani hujui kuwa huyu ni between the line...... ile ya MEI 15 mwaka huu na jiko, soma hapo chini kwenye blogu hii. uwe unauliza Lol......... na kama NAMTAKA WEWE INAKUHUSUJE??? Lol ha ha aha ha ha ha ha ha ha ha ha

  ReplyDelete

Maoni yako