July 21, 2010

HARUNA MOSHI YUKO SAHIHI?

Ukiniambia nimlaumu HARUNA MOSHI kuamua kuondoka nchini Sweden katika klabu ya Gefle nitakwambia, kosa lake ni lipi? Ukiniambia alikuwa akilipwa kwanini kaondoka nitakwambia acha afanye anachoona bora. JE YUKO SAHIHI AU HAYUKO SAHIHI?

2 comments:

 1. Ni yeye tu anajua kama yupo sahihi au hayupo sahihi:-)

  ReplyDelete
 2. kama ulivyosema haruna amefanya anachoona ni bora.

  mimi ni miongoni mwa tuliosikitika na kukatisha mkataba kwake. kwa mimi sio kwa sababu anarudi simba na hivyo kuimarisha kikosi kutufunga sisi yanga. la hasha mwaka huu simba hata wamkodi beki wa uruguay suarez mipira wataiona kwenye nyavu zao.

  wakoloni walitanguliza wamisionari, wafanyabiashara na wapelelezi. wakafanikiwa. kisoka la tanzania, haruna alikuwa mtangulizi wa professional footbal. wazungu hupendela kuscout wachezaji katika nchi ambazo tayali kuna wachezaji wa kulipwa. kurudi kwa haruna kunafanya mlango wa soka la kulipwa kuwa dogo zaidi. wachezaji wa nigeria kwa mfano hutafutiwa timu ulaya na wenzao walio ulaya.

  kuna sababu kadhaa zinasemwasemwa kuhusu haruna kukatisha soka ya kulipwa

  one school of thought inasema ni shinikizo la mkewe. zinatonya kuwa haruna alikaa sweden kwa muda mrefu kabla hajamchukua mkewe. ni hivi majuzi tu alikuja kumchukua mkwewe na punde si punde hao wanarudi tz. zinatonya kuwa mkewe alikuwa amemis mashoga zake sinza, alimisi miugali na joto la dar es salaam. sweden alishindwa baridi, lugha na vyakula. si mnajua behind any successful man there is a woman. inaweza kuwa kinyume chake pia.

  another school of thought inasema haruna hakutaka kukatwa kodi. ulaya soka ni kama kazi zingine na hivyo lazima mchezaji ukatwe kodi (TRA wajifunze kitu hapa). haruna alizani sweden ni mteremko kama bongo akaona ushenzikukatwa kodi na kurejea bongo.

  shule nyingine ya fikra inatonya kuwa wakuu wa klabu yake ya Geffe walimwita na kumwambia kiwango kimeshuka na hivyo kabla hawajamtimua ni heri ajitimue kimyakimya. eti ilifanyika hivo kulinda heshima ya boban kutomtupia virago.

  school of thought ya wasela inadai boban alimis ile dawa anayotumia bongo. sweden hakuna hata vijiwe vya kujidunga na hivyo kujisikia vibaya. ninamaanisha 'mboga za majani'

  ReplyDelete

Maoni yako