September 17, 2010

KOERO BINTI MKUNDI; NINAYO SIRI.....

Nilipoanza kuandika hapa, niliwaza sana. NA kwakuwa napenda kuwaza kwa uhuru na kusema kwa uhuru basi nakwambia Koero sijaribu kucheza kamari wala sijaribu kufanya amali za kubahatisha. KOERO BINTI MKUNDI, naomba TUOANE SASA.

Ingawaje wajua kuwa kila mtu anayosifa yake ya KUKUNG'OA KWENU, lakini kwa sifa ulizoandika KIJIJINI kwako VUKANI, lakini mie nasema kama awali kuwa dhamira yangu ni zaidi ya imani kwa JAH. Ni zaidi ya simulizi za Giningi. Ni zaidi ya MVUMILIVU HULA MBOVU.

Ni zaidi ya utani ujuao, lakini kwa hakika ninayo siri moyoni. Najua hujui ni siri gani, lakini nimekuja rasmi, sasa na kama ulikuwa unadhani natania naomba USIJARIBU. Utamu wa kula ni kuonja, kumbuka kula nanasi kwahitaji nafasi, ndiyo kama vile naiona ndiyo katika simulizi za SIYO.

Alfajiri nawaza, kila ukicha nawaza, ni lini nitakuwa wako yaani mimi peke yangu. Na kama ningeweza sasa, naamini ningekuja hima hata kama sina AMALI. Shughuli ya kwanza ni kwamba NINAYO SIRI MOYONI nitakwambia siku tukiweka kitako na kuongelea ya moyoni siyo yale ya kula na kushiba MAKANDE na ujuzi MSHAZARI.

Wajua kuwa Padre asiyehitimu ni MWOGA  wa mabinti na wajua kuwa ALFAJIRI ya ujumbe wako inanipa HISIA  zaidi ya DINARI AU RUPIA? Basi Koero angalia hili neno, NAKUPENDA KWA DHATI bila kushika manati, hakina sina HILA.

 Najua unaweza kushindwa kujua wapi, lakini tusitumie tu uwezo wa wamang'ati. Sina sheria kama mfalme Hammurabi, lakini NINALO PENZI MAHUSUSI KWAKO KOERO BINTI MKUNDI. Nalihifadhi PENZI HILO, siku ukipata nauli NITAFARIJIKA NIKIWA MIMI NDIYO MWISHO WA RELI.

NATAMBUA PENZI LA NDOA NI TAMU HALINA KIFICHO

7 comments:

  1. wenga ujovesa ganaga?
    kaazi kawelikweli !!

    ReplyDelete
  2. Koero huyu jamaa hana lolote....ukiona mtu anaongea sana ujuwe hajiamini.....utaumia bure.

    ReplyDelete
  3. Naona unajipigia debe kila kona, kwa taarifa yako humpati, maana umezidi maneno meeeengi.....

    ReplyDelete
  4. Koero mwenyewe siku hizi yuko kimyaaaaaa!!! Pengine wewe na Fadhy Mtanga ndiyo wa kulaumiwa. Tunamtaka Koero wetu arudi uwanjani mara moja; na kama kuna mmoja wenu ambaye "amemtorosha" basi amrudishe mara moja. Hata mahubiri ya Sabato kila Jumamosi hatupati tena. Wanaume nyie balaa tupu ati!

    ReplyDelete
  5. muveka na picha sa mganda

    ReplyDelete
  6. muveka na picha sa mganda jamani

    ReplyDelete

Maoni yako